Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombi Ya Kusudi Katika Ndoa YakoMfano

Maombi Ya Kusudi Katika Ndoa Yako

SIKU 4 YA 6

Ngao Ya Imani

"Kuwa na ndoa ambapo wenzi wote wawili wanatimiza kusudi lao haimaanishi kuwa kila wakati kutakuwepo kengele na tarumbeta. Inamaanisha kwamba imani katika wito na mwongozo wa Mungu kwa ajili yenu wenyewe, na kwa ajili ya kila mmoja wenu, mara nyingi itawapitisha katika nyakati zisizosisimua zinazotokea nazo huonekana kuwa za kawaida katika maisha ya kila mtu.” Tony Evans

Mungu Mpendwa, ni rahisi kuhoji kusudi na mwelekeo wa mambo yanapochelewa. Ni rahisi hasa ikiwa kuchelewa huko kwa sababisha aina yoyote ya taabu nyumbani, usumbufu au hata hasara ya kifedha ya aina fulani. Mara nyingi ucheleweshaji huu unaweza kugeuka kuwa shaka. Na mashaka yanaweza kusababisha mgawanyiko tunapoulizana maswali sisi kwa sisi na kusudi lako katika maisha ya kila mmoja wetu.

Bwana, tusaidie kujitolea kikamilifu kukuona ukitekeleza kusudi lako kwa kila mmoja wetu binafsi, na kwa ajili yetu pamoja kama wanandoa katika wakati wako. Tupe subira wakati mambo hayaonekani kuwa yanakwenda sawa sawa. Utusaidie tuichukue ngao ya imani inayotukumbusha kuwa maono bado itatimia kwa wakati ulioamriwa, na hadi wakati huo utakapofika, Mungu, tunapaswa kutumikiana kwa unyenyekevu, kutiana moyo na kuelewana.

Imani ya mwenzi wangu inapopungua kwa sababu ya kucheleweshwa na kupotoka kuelekea kusudi lao - nisaidie kuwa hapo ili kuwakumbusha kukutumaini wewe kwa imani. Na mwenzi wangu anifanyie vivyo hivyo wakati ambapo imani yangu inadhoofika. Kuna siku ambazo mmoja wetu ana nguvu na mwingine hana—wakati mmoja wetu ana imani isiyoyumba na maono ya siku zijazo na mwingine hana. Hebu tuweze kusifiana.mmoja na mwingine, tuwe wakuinuana kiimani iwe kwa maombi, maneno ya kutia moyo au kwa kutolalamika tu pale mambo yanapoonekana kwenda mrama katika safari hii ya kuelekea kusudi. Kati yetu sisi wawili, tusaidie kusawazishana kila mmoja na mwingine ili imani yetu ibaki kuwa imara kwa pamoja na kwa muda mrefu. Katika jina la Kristo, amina.

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Maombi Ya Kusudi Katika Ndoa Yako

Kamwe katika historia ya ulimwengu taasisi ya ndoa haijawahi kuwa chini ya chunguzi kama ilivyo. Kila siku, jamii hutafuta kufafanua upya maana ya kuoa, na Wakristo wanakabiliwa na ukosoaji mkubwa zaidi kwa kushikilia kile kinachoitwa mtazamo na wa mawazo finyu kuhusu ndoa. Kwa hivyo kusudi la kibiblia la ndoa ni nini, na tunapaswa kuombaje kama waumini ili kuhifadhi maana yake? Katika kampeni yetu ya siku sita, Maombi ya Kusudi katika Ndoa Yako, wanandoa wanaweza kuomba kuwepo na maana katika ndoa yao wenyewe, na pia kuthibitisha ufahamu wa kimungu wa muungano wa agano kati ya mwanamume na mwanamke.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/