Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

KubarikiwaMfano

Blessed

SIKU 2 YA 7

"Baraka"

"Heri mtu (mwenye furaha, mwenye bahati, anayeonewa wivu) anayemcha(anaheshimu na kuabudu) Mwenyezi-Mungu" hivyo ndivyo Biblia inasema katika mstari wa kwanza wa Zaburi 112. 

Kote katika Biblia, Mungu anaahidi mara kwa mara kubariki watu wake, lakini baraka zake pia zinategemea chaguo zetu. Anaweka chaguo mbili za wazi kwa watu: "Naziita mbingu na dunia zishuhudie juu yenu leo hii, kwamba nimewapeni uchaguzi kati ya uhai na kifo, kati ya baraka na laana. Basi chagueni uhai nyinyi na wazawa wenu mpate kuishi" (Kumbukumbu la Torati 30:19). 

Kitabu cha Kumbukumbu la Torati katika Agano la Kale kina orodha za baraka na orodha za laana ambazo zilikuwa zinahusishwa moja kwa moja ikiwa mtu atachagua kutii au kutotii amri za Bwana. Unaweza kusoma hayo yote katika Kumbukumbu la Torati 28:1-14, lakini elewa ya kwamba kuchagua maisha na Mungu ni kuchagua maisha yaliyobarikiwa. Nia ya Mungu kila mara ni kukubariki, lakini ukidhani kuwa baraka zake ni za kwako zote, unakosa  uhakika. 

Baraka za Mungu maishani mwako zinafaa kwenda zaidi ya uwepo wako mwenyewe. Mungu alimwambia Ibrahimu kuwa angembariki, lakini lengo la kumbariki lilikwenda mbali zaidi na maisha yake mwenyewe. Hivi ndivyo Mungu alisema: 

"Nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa; nitakubariki na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka" (Mwanzo 12:2).

Lengo la baraka za Mungu ni kukuwezesha kuwa mfereji wa baraka kwa wengine. Kama huna chochote, hakuna unachoweza fanyia mtu yeyote; Kama una kichache, unaweza saidia tu kidogo; lakini kama una mengi , kuna mengi unayoweza fanya. Unapobarikiwa, una msingi imara ambao unaweza kutumia kushawishi wengine. Unabarikiwa ili uwe baraka. 

NYANJA YA MAISHA YAKO
Nia ya Mungu ni kukubariki, kwa hivyo weka moyo wako ili umheshimu katika sehemu yoyote ile ya siku yako. Chagua maisha, na uwe baraka kwa watu ambao Mungu ameweka katika kila nyanja ya ushawishi wako!

Kuhusu Mpango huu

Blessed

Unaishi vipi maisha yaliyo barikiwa? Naamini kila mtu anahamu na anatafuta jibu hili. Miongoni mwa wahusika mbalimbali katika Biblia, kuna mmoja hasa ambaye napenda. Jina lake halijatajwa, lakini anaishi kwa kanuni za Biblia. Huyu shujaa wangu wa Kibiblia ndiye mtu mwema aliyetajwa katika Zaburi 112.

More

Tungependa kuwashukuru Brian Houston na Hillsong kwa kutoa huu mpango. Kwa maelezo zaidi, tembelea: http://BrianCHouston.com