KubarikiwaMfano
"Bwana Asifiwe"
Bwana Asifiwe! Ndani ya maneno hayo matatu ni mwanzo wa nguvu na msingi wa maisha yaliyobarikiwa. Inaanza kwa kumjua Mungu ni nani na kumsifu.
Sifa ndio mwanzo daima. Inamaanisha shukrani—ndio maana sisi hutoa shukrani kabla ya mlo na kuanza kanisa na nyimbo za sifa. Yesu alianza kumshukuru Mungu kabla ya Lazaro kufufuliwa kutoka kwa wafu, na Musa alimsifu Mungu kabla ya kugawanya Bahari Nyekundu. Asili ya binadamu ni kungoja baada ya kupata jibu, lakini baraka huanza na sifa.
Neno la Mungu linasema, "Ingieni katika lango lake kwa shukrani, na nyuani mwake kwa kumsifu" (Zaburi 100:4) Ilhali kumsifu Bwana sio tu kuimba nyimbo chache mara moja kwa wiki kanisani. Kuabudu ni hali ya maisha ambayo hukumbatia maisha yote kwa jumla.
Unaweza kumsifu Mungu wakati wowote wa siku, siku saba za wiki— kwenye gari, kwenye bafu au usiku wa manane. Sio tu kuimba wimbo wa kidini fulani au kukariri ombi — ni kuhusu uhusiano na Baba wako wa Mbiguni ambaye anakupenda na anakujali.
Watu wana mawazo tofauti juu ya Mungu, na wanawasiliana naye kwa mujibu wa mitazamo yao. Wale ambao wanadhani ni mgumu na mkali wamemuweka mbali. Wengine, ambao wanamuona kuwa rasmi na madhubuti, kawaida wanamkaribia kwa njia hiyo hiyo. Ilhali wale ambao wanamjua kama Baba na Rafiki wanafurahia
baraka za uhusiano wa karibu na wa kimapenzi naye — pale ambapo unaweza muita wakati wowote. Haijalishi uko katika hali gani, kamwe hauko peke yako.
Hali huanza kubadilika unapoanza kumsifu bwana. Sifa haimuweki
katika lengo, lakini inakufanya uone vitu katika mtazamo mpya.
Kumsifu Mungu ni zaidi ya sherehe ya mila au tukio la mara moja. Ni namna ya maisha ya kuabudu — hukuwezesha kuweka lengo lako kwa Mungu, na hubadilisha mtazamo wako wa hali uliyoko. Kwa hivyo nenda leo katika wito uliopewa na Mungu na tamko hili kama msingi wako:
"Bwana Asifiwe!"

Kuhusu Mpango huu
Unaishi vipi maisha yaliyo barikiwa? Naamini kila mtu anahamu na anatafuta jibu hili. Miongoni mwa wahusika mbalimbali katika Biblia, kuna mmoja hasa ambaye napenda. Jina lake halijatajwa, lakini anaishi kwa kanuni za Biblia. Huyu shujaa wangu wa Kibiblia ndiye mtu mwema aliyetajwa katika Zaburi 112.
More
Tungependa kuwashukuru Brian Houston na Hillsong kwa kutoa huu mpango. Kwa maelezo zaidi, tembelea: http://BrianCHouston.com