Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano
Ni sifa za mtawala mwema aliye na haki katika tabia na matendo yake. Awajibika katika kuwatetea walioonewa akiwapinga wahalifu wanaoonea watu. Ni kama mvua ilivyo kwa nchi. Atahakikisha ufalme wake unaleta furaha, mafanikio, amani na maisha ya heri. Tena ufalme wake utakuwa hauna mipaka. Tukitafakari sifa hizo zote tunaelewa zaburi hii inatoa unabii unaomhusu Masihi, mfalme wa pekee wa ukoo wa Daudi. Huyu ndiye Yesu aliyetimiza yote yaliyotajwa katika maombi haya. Yn 12:14-15 ni habari moja inayothibitisha hiyo: Naye Yesu alikuwa amepata mwana-punda, akampanda, kama vile iliyoandikwa, Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda. - Tumsujudie!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/