Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 11 YA 31

Angalia, Mungu ndiye aliyelitakasa hekalu. Katika m.3 (na vivyo hivyo katika m.7) anasema, Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu huko milele. Sasa anamkumbusha Sulemani kutunza utakatifu huu. Waisraeli waendelee kumtegemea Mungu kwa moyo, na wawe waaminifu katika kuzitii amri zake. Hii itufundishe kuwa pamoja na kujenga makanisa mazuri, kufika kuabudu, kutoa sadaka kwa uaminifu, lakini Mungu anataka tumpende na kumtii. Kama tusipomtii na kumfuata katika roho na kweli, tunazuia ahadi za Mungu zisitimilike kwetu, naye atatuacha. Zingatia Yesu anavyosema, Mkinipenda, mtazishika amri zangu; Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake (Yn 14:15, 21). Na tena anasema, Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu. Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake (Yn 15:9-10).

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/