Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano
Pamoja na mazuri tuliyojifunza kwa Sulemani, tuzingatie pia tatizo alilojipatia. Kinyume na maagizo yaliyo wazi ya Mungu, alioa wake wengi na kutoka makabila mbalimbali. Kwa hiyo alivunja sheria inayosema kwamba asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke (Kum 17:17). Matokeo yake, wanawake hao wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine (m.4). Tabia hizi zipo hata leo. Wapo watu ambao wakifanikiwa kiuchumi au kiuongozi, huanza kufanya yasiyofaa, k.mf. kuoa wanawake wengi, kuwadanganya wasichana au kutumia madaraka yao kunyanyasa wanyonge. Hayo yote ni mabaya mbele za Mungu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/