Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano
Yohana alihubiri hukumu ya Mungu bila kuficha. Alionya kuna hasira itakayokuja, kwa hiyo mtu asiyetubu atatupwa kwenye moto usiozimika. Mahubiri hayo yalikusudia watu waamke, na wakishaamka waje kwa Mungu ili kusamehewa dhambi zao. Hili ni jambo la pekee alilolitenda Yohana: Alihubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi (m.3). Kama angalifuata kawaida yao angaliwatuma hekaluni ili waondolewe dhambi zao kwa utoaji sadaka. Lakini sivyo. Hii ni dalili ya majira mapya kukaribia! Ndivyo alivyotabiri Zekaria, baba yake: Uwajulishe watu wake wokovu, Katika kusamehewa dhambi zao (1:77).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/