Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano
Yesu ni Mwisraeli, ni Myahudi. Mama yake ni Myahudi na baba yake wa kambo ni Myahudi. Kwa hiyo twasoma kuwa baada ya kuzaliwa alifanyiwa kutokana na sheria waliyopewa Wayahudi (m.39, Walipokwisha kuyatimiza yote kama yalivyoagizwa katika sheria ya Bwana, walirejea Galilaya mpaka mjini kwao, Nazareti). Alitahiriwa baada ya siku nane (m.21, Hata zilipotumia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu), na alitolewa sadaka hekaluni Yerusalemu (m.22-24, Zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo torati ya Musa walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana, (kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, Kila mtoto mwanamume aliye kifungua mimba ya mamaye na aitwe mtakatifu kwa Bwana), wakatoe na sadaka, kama ilivyonenwa katika sheria ya Bwana, Hua wawili au makinda ya njiwa wawili. Kuhusu sadaka hiyo unaweza kusoma zaidi katika Kut 13:2, 12, 15-16; 34:19-20 na Law 5:7; 12:8). Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria (Gal 4:4). Hiyo ni sehemu ya maana ya habari katika Yn 1:11 kwamba alikuja kwake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/