Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano
Zekaria anashirikishwa hali ya jamii iliyopo wakati wake. “Pembe” ni mfano wa nguvu na kutoa picha ya maadui wa watu wa Mungu. Kuna mazungumzo baina ya Zekaria na Mungu. Maono yanahusu uharibifu ulioletwa na hao maadui. Watu wa Mungu wametawanyika huku na huko. Hawapo walipokusudiwa wawepo. Lakini Mungu ana mpango mkakati wa wazi uhusikao na kuwarudisha mahali pao pa asili (m.20-21, Bwana akanionyesha wafua chuma wanne. … Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, hata ikawa hakuna mtu aliyeinua kichwa chake; lakini hawa wamekuja kuzifukuza, kuziangusha pembe za mataifa, walioinua pembe yao juu ya nchi ya Yuda, ili kuwatawanya watu wake). Hajawahi kuuacha uovu uendelee pasipo kuingilia kati. Hakuna uovu wa kudumu. Nguvu ya Bwana itatawala tu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/