Upendo wa Kweli ni nini?Mfano
Lengo Kuu
Kama upendo wa kweli ndio lengo kuu, mbona tusitake kujua unavyofwanana na jinsi ya kupata upendo huu? Swali tutakalo jiuliza ni, je tunaweza jua upendo wa kweli?Kama Mungu ni Upendo,
na Mungu anatuamuru tumpende,
na Mungu, kwa neema, ameweka upendo wake mioyoni mwetu kupitia Kristo katika wokovu wetu,
basi tunaweza kuhitimisha kuwa jibu ni ndio—NDIO iliyothabiti!
Tumepewa uwezo wa kujua upendo wa kweli, kufurahia upendo wa kweli, kuishi kwa upendo wa kweli, na kutoa upendo wa kweli. Kama Mungu mwenyewe ni upendo, basi yeye sio tu mfano na kiwango cha upendo, lakini yeye mwenyewe ni chanzo vile vile.
Lakini je, kuna vikwazo ambavyo vinaweza tuzuia?
Kutoamini? maumivu? Usaliti? Kukosa tumaini? Kutojali? Kazi? Nyumbani? Umaarufu? Uoga? Kutokuwa na thamani? Kushindwa? Yafikirie haya leo ukiwa kazini, nyumbani, ukiendesha gari ... kisha nenda mbele zake Mungu kwa maombi, mwambie yale ambayo umegundua. Ukihisi kana kwamba kuna kikwazo, lakini pia hauko karibu unavyotakikana, mwambie Bwana vile vile.

Kuhusu Mpango huu
Kila mtu anataka kujua upendo ni kitu gani. Lakini watu wachache huangalia ni nini Biblia inasema kuhusu upendo. Upendo ni mada moja muhimu ya Maandiko na pia wema muhimu zaidi katika maisha ya Kikristo. Mpango huu kutoka Huduma za Thistlebend unashughulikia maana ya kibiblia ya upendo na jinsi ya kuboresha kumpenda Mungu na kuwapenda wengine.
More
Tungependa kushukuru huduma za Thistlebend kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.thistlebendministries.org