Upendo wa Kweli ni nini?Mfano
Kutamani Upendo
Mioyo yetu sisi sote inatamani upendo haijalishi kama tunajua au hatutambui. Tuliumbwa haswa kupenda. Mungu ni Upendo. Je, unatamani kujua upendo wa kweli wa Mungu? Kisha, unatamani kumpenda kiukweli kwa moyo wako wote, nafsi yako yote, akili na nguvu kwa upande wako.Lakini upendo wa kweli ni nini? Neno hilo lina maana nyingi. Tunaweza sema kwa pumzi moja, "Napenda kahawa. Nampenda mume/mke wangu. Nampenda Yesu." Ni vipi tunaweza tambua upendo wa kweli ni nini? Unafuanana na nini? Ni kuhisi vipi? NI muhimu?Upendo wa kweli ni zaidi ya hisia, misheni au hata mafundisho. Upendo wa kweli ni hamu ya kweli ya kuona mwenzako anastawi. Upendo wa kweli unaoleta utukufu kwa Mungu ndio madhumuni hasa ya maisha na uwepo wa kanisa.
Wengine watasema misheni ndio lengo muhimu la kanisa: "Lengo kuu la Kanisa ni uinjilisti ulimwenguni. Ujume na kazi ya Kanisa ni misheni"(Oswald J. Smith).
Wengine watasema ni kuabudu: "Misheni sio lengo kuu la kanisa. Ni kuabudu. Misheni zipo kwa sababu kuabudu hakupo. Kuabudu ndoi swala kuu, sio misheni, kwa sababu Mungu ndie Mkuu wala sio binadamu. Wakati kizazi hiki kitaisha, na mamilioni ya waliokombolewa wakiinamisha nyuso zao mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, misheni zitakuwa zimemalizika. Ni haja ya muda mfupi. Lakini kuabudu kutadumu milele" (John Piper).
Ninakudokezea kuwa upendo ni swala kuu na kuwa misheni na kuabudu ni matawi ya huo upendo. Mungu anawaamrisha watu wake wampende kwa mioyo, nafsi na nguvu zao zote. Yesu anasisitiza haya, anatuambia kuwa amri ya kwanza na kuu ni kumpenda Bwana Mungu wetu kwa moyo wetu WOTE, nafsi yetu YOTE, akili yetu YOTE na nguvu zetu ZOTE. YOTE kumaanisha YOTE. Baadaye anatuambia kuwa watu watajua kuwa sisi ni wanafunzi wake kwa upendo wetu tunaowaonyesha wengine. Kisha Paulo anaelezea katika barua yake kwa Wakorinthokuwa imani, na upendo ni fadhila za kudumu, lakini kubwa ya haya matatu ni upendo. Kulingana na Mungu, Yesu na Paulo, upendo unaonekana kuwa lengo kuu kwetu na pia vile vile kwa kanisa.

Kuhusu Mpango huu
Kila mtu anataka kujua upendo ni kitu gani. Lakini watu wachache huangalia ni nini Biblia inasema kuhusu upendo. Upendo ni mada moja muhimu ya Maandiko na pia wema muhimu zaidi katika maisha ya Kikristo. Mpango huu kutoka Huduma za Thistlebend unashughulikia maana ya kibiblia ya upendo na jinsi ya kuboresha kumpenda Mungu na kuwapenda wengine.
More
Tungependa kushukuru huduma za Thistlebend kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.thistlebendministries.org