BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumeMfano
Katika sehemu inayofuata ya Matendo ya Mitume, Paulo anagundua kuwa kuna baadhi ya Wakristo Wayahudi ambao wanang'ang'ana kuwa Wakristo wasio Wayahudi ni lazima wawe Wayahudi (kwa kufanya tohara, kutunza Sabato, na kutimiza sheria za chakula za Kiyahudi) ili kuwa sehemu ya vuguvugu ya Yesu. Lakini Paulo na Barnaba wanakataa kabisa, na wanapeleka mjadala huu mbele ya baraza la uongozi huko Yerusalemu ili utatuliwe. Wakiwa huko, Petro, Paulo na Yakobo (kaka wa Yesu) wanarejelea Maandishi na uzoefu wao binafsi ili kuonyesha kuwa mpango wa Mungu daima umekuwa kujumuisha mataifa yote. Kisha baraza linafanya uamuzi bunifu na kuweka wazi kuwa japo ni lazima Wakristo ambao si Wayahudi kuacha kushiriki katika kafara za mahekalu ya kipagani, hawahitaji kuchukua utambulisho wa kikabila wa Kiyahudi au kutii sheria za ibada na desturi za Torati. Yesu ndiye Masihi wa Kiyahudi, lakini yeye pia ndiye Mfalme aliyefufuka wa mataifa yote. Uanachama katika Ufalme wa Mungu hauna misingi katika ukabila au sheria ila tu kumwamini na kumtii Yesu.
Soma, Tafakari, kisha Ujibu:
• Ni mawazo, maswali, au maarifa yapi yaliibuka ulivyokuwa unasoma sura ya leo?
•Unafikiri nini kingefanyika iwapo Paulo na Barnaba wangeepuka mgogoro na walimu kutoka Yudea (15:1-2)? Unafikiri ni kwa nini walizungumza na kuendeleza mjadala thabiti hivyo? Matokeo ya mara moja ya makubaliano yao yaliyoongozwa na Roho yalikuwa yapi (tazama 15:31)? Je, kuna mtu yeyote katika jamii yako anahisi ametengwa kwa njia isiyo ya haki? Unawezaje kuanzisha mgogoro chanya kwa niaba yake?
• Acha tafakari yako ichochee maombi. Mshukuru Yesu kwa kujumuisha wote wanaomwamini. Muombe akuonyeshe palipo na vizuizi ambavyo vinawatenga au kuwasumbua watu katika jamii yako. Omba kupata ujasiri wa kuongea na kutetea kilicho kweli na upendo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com