Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mdo 15

15
Baraza la Yerusalemu
1 # Law 12:3; Gal 5:2 Wakashuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka. 2#Mdo 11:30; Gal 2:1Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee kwa habari ya swali hilo.
3Basi, wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya nchi ya Foinike na Samaria, wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana. 4#Mdo 14:27Walipofika Yerusalemu wakakaribishwa na kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao. 5Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika torati ya Musa.
6Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neno hilo. 7#Mdo 10:1-43; 11:15Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba Mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini. 8#Mdo 2:4; 10:44Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi; 9#Mdo 10:34wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani. 10#Gal 3:10; 5:1; Mt 11:30Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua. 11#Gal 2:16; Efe 2:4-10Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.
12Basi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paulo wakiwapasha habari za ishara na maajabu, ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika Mataifa. 13#Mdo 21:18; Gal 2:9Na hao walipokwisha kunyamaza Yakobo akajibu, akisema, Ndugu zangu, nisikilizeni.
14 # Mdo 15:7-9; Lk 1:68 Simeoni ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza alivyowaangalia Mataifa ili achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake. 15#Amo 9:11,12Na maneno ya manabii yapatana na hayo, kama ilivyoandikwa,
16 # Amo 9:11-12; Yer 12:15 Baada ya mambo haya nitarejea,
Nami nitaijenga tena nyumba ya Daudi iliyoanguka.
Nitajenga tena maanguko yake,
Nami nitaisimamisha;
17Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana,
Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao;
18 # Isa 45:21 Asema Bwana, ajulishaye hayo tangu milele.
19Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi; Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa; 20#Kut 34:15-17; Law 3:17; 5:2; 17:10-16; 18:6-23; Mwa 9:4bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu. 21#Mdo 13:15Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi.
Barua ya Baraza kwa Waumini wa Mataifa
22Basi ikawapendeza mitume na wazee na kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba; nao ni hawa, Yuda aliyeitwa Barsaba, na Sila, waliokuwa watu wakuu katika ndugu. Wakaandika hivi na kupeleka kwa mikono yao,
23Mitume na ndugu wazee, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shamu na Kilikia, walio wa Mataifa; Salamu. 24#Mdo 15:1Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbua kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, ambao sisi hatukuwaagiza; 25sisi tumeona vema, hali tumepatana kwa moyo mmoja, kuwachagua watu na kuwapeleka kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paulo, 26watu waliohatirisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana wetu Yesu Kristo. 27Basi tumewatuma Yuda na Sila, watakaowaambia wenyewe maneno yayo hayo kwa vinywa vyao. 28#Mt 23:4Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo lazima, 29yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu.
30Hata hao wakiisha kupewa ruhusa wakatelemkia Antiokia; na baada ya kuwakusanya jamii yote wakawapa ile barua. 31Nao walipokwisha kuisoma wakafurahi kwa ajili ya faraja ile. 32#Mdo 11:27; 13:1Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathibitisha. 33Na wakiisha kukaa huko muda, wakaruhusiwa na ndugu waende kwa amani kwa hao waliowatuma.
[ 34Lakini Sila akaona vema kukaa huko.] 35Na Paulo na Barnaba wakakaa huko Antiokia, wakifundisha na kulihubiri neno la Bwana, pamoja na watu wengine wengi.
Paulo na Barnaba Watengana
36 # 1 The 3:5 Baada ya siku kadha wa kadha Paulo akamwambia Barnaba, Haya! Mrejee sasa tukawaangalie hao ndugu katika kila mji tulipolihubiri neno la Bwana, wa hali gani. 37#Mdo 12:12,25Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja nao. 38#Mdo 13:13; Kol 4:10Bali Paulo hakuona vema kumchukua huyo aliyewaacha huko Pamfilia, asiende nao kazini. 39#Mdo 4:36; 13:4Basi palitokea mashindano baina yao hata wakatengana. Barnaba akamchukua Marko akatweka kwenda Kipro. 40Lakini Paulo akamchagua Sila, akaondoka, akiombewa na wale ndugu apewe neema ya Bwana. 41Akapita katika Shamu na Kilikia akiyathibitisha makanisa.

Iliyochaguliwa sasa

Mdo 15: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia