Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021Mfano
Yesu ni Bwana wa mavuno (katika m.14 anatambulishwa kama mfano wa Mwanadamu ... na katika mkono wake mundu mkali). Hapa mavuno yamelinganishwa na siku ya mwisho. Je, itakuwaje siku hiyo? Japo sisi sote ni kama magugu na ngano vilivyokua pamoja, dhahiri shahiri siku hiyo itaonyesha tofauti iliyopo: Itatokea na hukumu kwao wasioamini (hiyo inafafanuliwa kwa njia ya mfano katika m.19-20 kama shinikizo ... kubwa la ghadhabu ya Mungu, wasioamini wakiwa zabibu zinazotupwa katika shinikizo hilo), wakati Yesu atakapojishughulisha kipekee na kazi ya kuwakusanya waumini ghalani mwake kwa uzima na furaha ya milele (ni maana ya nchi ikavunwa katika m.16). Je, mimi na wewe ni ngano au magugu? Bwana Yesu asifiwe! Aweza kutufanya ngano sasa hivi tukimwamini.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/