Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021Mfano
Tokeo la vita kati ya mpinga Kristo (13:1nk) na Kristo (14:1nk) lajulikana tayari, maana habari yake imeshaandikwa katika Injili ya milele (m.6): Kumfuata Yesu ni pamoja na taabu na kifo, na lazima kusubiri ushindi (m.12, Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu). Lakini matokeo ya kumwacha na kugeukia kumwabudu mwingine ni sawa na kuangukia katika hukumu ya milele ya Mungu. Na moshi ya maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake (m.11). Na mfumo unaoendeleza hayo, yaani Babeli, mji ule ulio mkubwa, hakika umeanguka (m.8)! Wewe uko wapi? Katika Babeli kwa waabudu shetani na sanamu? Au kwa wenye hekima wamchao Mungu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/