Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021Mfano
Tangu kushindwa na kutupwa duniani, shetani hajapoteza wakati. Hima akaanza kumfuatilia yule mwanamke (= waumini wa agano la kale) ili amwangamize. Vivyo hivyo siku hizi hajatulia. Kama simba angurumaye, shetani daima huzunguka akitafuta kuwaangamiza waaminio (1 Pet 5:8). Lakini asante Mungu, maana aweza kuwahifadhi ndani ya wokovu ule aliotufanyia kwa njia ya kumwamini Yesu. Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na husu ya wakati mbali na nyoka huyo. ... Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake (m.14 na 16). Swali kwako sasa ni: Je, wamwamini Yesu? Mwamini, usishindwe na mashambulizi ya joka!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/