Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021Mfano
Zaburi hii inaeleza njia ya haki ya Mungu na maisha ya kila siku waishiyo waumini na Bwana wao. Usitafute kuishi hivyo ili kuingia kwa Mungu, maana tunaingia kwa njia ya kumwamini Yesu. Lakini hali umeokoka, basi tafuta kuishi unavyoelezwa hapo, maana mtu atendaye mambo hayo hataondoshwa milele kutoka kukaa na Bwana (m.15)! Kumtafuta Yesu kunahitaji kujipima dhidi ya matendo yasiyo haki. Anza na moyo (m.2), maana hapo hutoka uzima, na Zaburi inatuangaliza kuhusu kuwa na ukamilifu wa moyo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/