Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021Mfano
Unyenyekevu wako umenikuza (m.36). Tungeweza kuitafsiri kauli hii kwa hivi: Kuinama kwako kumenifanya mkuu. Kufanikiwa kwa Daudi wakati wa shida na taabu si kutokana na uwezo wake mwenyewe, bali ni kwa sababu ya msaada wa Mungu tu. Daudi hakustahili kwamba Mungu mwenye enzi yote akubali kujishughulisha na mapambano yake. Lakini katika uaminifu wake, Bwana akakubali, akanyosha mkono wake mwenye nguvu kutoka juu, akamshindia Daudi, akamtoa, akampeleka panapo nafasi. Alipeleka kutoka juu, akanishika; Akanitoa katika maji mengi. ... Akanitoa akanipeleka panapo nafasi; Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami (22:17,20).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/