Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021Mfano
Dunia ikatetemeka na kutikisika, misingi ya mbinguni ikayumbayumba na kuruka, kwani Mungu alikuwa amekasirika (m.8 BHN). Hapa tunajifunza mambo matatu: 1. Mungu ana mamlaka yote juu ya mbingu na nchi. 2. Mtu wa Mungu akiomba, ndipo Mungu huanza kufanya kazi kwa nguvu zake za ajabu (Daudi anasema Mungu akiisikia sauti yake, ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka; m.7-8). 3. Mungu yuko macho sana katika kuwalinda watu wake. - Hii ni raha ya mtoto wa Mungu kwamba Mungu aliye na mamlaka yote yu pamoja naye na hakuna kitu kinachoweza kumdhuru. Ukiwa na nafasi, soma Yn 10:27-29 na Rum 8:35-39.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/