Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Silaha ya MunguMfano

The Armor of God

SIKU 4 YA 5

Katika historia yote ta vita, moja ya mbinu ya kivita iliyoundwa kwa ajili ya kuvuruga ilikuwa ni kuanzisha mashambulizi ya kushitukiza kwa mishale ya moto. Mishale hii, iliwashwa moto kwenye ncha, iliruka juu angani kuelekea kwenye kwenye lengo ( kwa mfano, magari ya maturubai na maturubai ya kambi ya kijeshi), kuunguza kila kitu.

Na, mwanadamu, hakufua dafu. Kama mishale hiyomya moto ilipiga malengo yakutosha, kikosi kizima cha askari kitakuwa na kazi ya kujaribu kuzima moto kabla haujateketeza vifaa vyote na chakula. Kusumbuliwa na moto, watu wanakuwa wahanga wa kutingwa, kusumbuliwa ili kuhangaika na kushughulikia na mipango ya mashambulizi ambayo adui alikuwa anapanga.

Mishale ya moto kimsingi haikukusudiwa kuua au kuharibu; ilikusudiwa kuvuruga. 

Adui yako anataka kukuvuruga, dada. Ili akupofushe. Na unisikilize-- siyo kwamba anarusha tuu hiyo mishale yake. Amepanga katika mbinu yake. Amesoma tabia zako na mwenendo wako, hofu yako kuu na udhaifu wako, na amekusudia maeneo hayo. Anajua hawezi kukuangamiza. Unalindwa milele na Yesu. Lakini amekusudia kabisa kuondoa usikivu wako kwenye reli kwa kuwasha mioto ya ndani maishani mwako-- kama kutokuwa salama, mashaka, uoga, au kuwa na shughuli nyingi. Anataka uchanganyikiwe wakati yeye anakunyatia kutoka nyuma./p>

Katiaka Waefeso 6, Paulo anatumia mkanda, dirii, na viatu kama vazi la kiroho ambalo linatakiwa kuvaliwa na waamini wakati wote. Dakika kwa dakika. Siku kwa siku. Lakini na ngao ya imani, anaagiza "itwaliwe."

Hebu itazame kwa namna hii: Mkunga anaweza kuvaa mavazi ya upasuaji kwenda kazini kwa sababu ni sare yake. Lakini hitaji linapotokea, anaweza kuchukua stetoskopi (manati), mashine ya kupimia mapigo ya moyo, au vifaa vyovyote kutumia kwa mgonjwa wake. Vivyo hivyo, lazima siku zote tuvae kila siku sare za kimungu tulizopewa, lakini pia tuwe tayari " kutwaa" zingine zinapohitajika.

Ya kwanza katika silaha hizi ni ngao ya imani. Mara tunapohisi mishale ya moto inaingilia maisha yetu kwa namna yoyote, tunaamsha imani kama ngao ya kulinda maisha yetu.

Usikose kejeli hapa. Adui hutuma mishale ya moto katika maisha yako mahususi unapoitwa kutembea kwa imani. Mishale hiyo kwa makusudi kukudhoofisha usifanye kitu pekee chenye nguvu ya kuizima: kutembea kwa imani! Imani hufanya mishale ya moto kuzima.

Mungu anachokuta ufanye? Fanya! Kwa Imani.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

The Armor of God

Kila siku, vita isiyoonekana inapiganwa kukuzunguka--haionekani, haisikiki, lakini bado unaihisi katika maisha yako yote. Adui wa kishetani aliyejitoa kuleta uharibifu kwa kila kitu muhimu kwako: moyo wako, akili yako, ndoa yako, watoto wako, ndoto zako, hatima yako. Lakini mpango wake wa vita unategemea kukustukiza wakati huna silaha za vita. Kama umechoka kusukumwa na kusitukizwa, somo hili ni kwa ajili yako.

More

Tungependa kuwashukuru Priscilla Shirer na LifeWay Christian Resources kwa kutupa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: www.lifeway.com