Soma Biblia Kila Siku Machi 2021Mfano
Ziko nyakati katika maisha ya waamini ambazo Mungu huonekana kana kwamba amejificha au hasikii. Hali hii hutokea hasa tunapoonewa na kudhulumiwa. Watutendeao hivyo hufurahi na kujigamba kuwa Mungu hatusikii wala hatawahukumu. Lakini wamtegemeao Mungu wasinaswe katika udanganyifu kuwa Mungu hatatenda. Zaburi hii itukumbushe kwamba binadamu ni udongo (m.18), lakini Bwana ndiye Mfalme wa milele na milele(m.16), na atalitega sikio lake kwa maombi ya wanyonge (m.17). Amwaminiye Mungu amtegemee neno la Hab 2:4, Mwenye haki ataishi kwa imani yake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz