Chuma Hunoa Chuma: Life-to-Life® Mentoring in the Old TestamentMfano
![Iron Sharpens Iron: Life-to-Life® Mentoring in the Old Testament](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F23762%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Siku 3: Naomi and Ruthu
Mungu kama alivyomtumia Musa kumfundisha Yoshua kama kiongozi ajaye wa watu wake, vivyo hivyo Mungu alimtumia Naomi kuwa sambamba na mkwewe Ruthu katika wakati muhimu na wa hatari katika maisha yake.
Tunasoma habari yao katika sura nne za kitabu cha Ruthu. Ilitokea katika siku za Waamuzi baada ya ya Waebrania kutulia katika nchi ya ahadi lakini kabla hawajamtawaza mfalme wao wa kwanza. Njaa katika nchi ilimuongoza mtu aliyeitwa Elimereki, mkewe, Naomi, na watoto wao wawili wa kiume kuhama kutoka Bethlehemu kwenda Moabu.
Muda mfupi baada ya kuhama, msiba uliwapata baada ya Elimeleki kufariki. Watoto wawili wa Naomi wakawaona wanawake wa Moabu na msiba ukawapata tena baada ya wale watoto wa kiume kufariki. Mke mmoja alibaki Moabu, wakati mwingine, Ruthu, alimfuata mama mkwe wake kurudi Bethlehemu.
Ruthu, mgeni katika Yuda, nchi ya mumewe, alikuwa karibu na Naomi, aliyekuja kuwa mwalimu wake. Unapofikiria hili, wawili wasingekuwa tofauti. Mmoja alikuwa mzee, na mwingine kijana. Walitoka katika kabila tofauti. tamaduni tofauti, na tofauti ya kidini.
Lakini katika kusoma habari yao, tunaona kutegemeana kwenye maana. Tunaona pia Ruthu akiingia kwenye agano la mahusiano na Naomi, ambalo lilihusisha Ruthu kujitoa kwa moyo wote: "Watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu. Pale utakapokufa nitakufa nami, na papo hapo nitazikwa. Bwana anitendee vivyo na kuzidi, ila kufa tu kutatutenga wewe nami."
Kama habari isemavyo, Naomi alitembea pamoja na Ruthu wakati Ruthu anakutana na kuingia kwenye mahusiano na mwanaume aliyeitwa Boazi. Mwalimu wake aliwaongoza Ruthu na Boazi kwenye ndoa. Ruthu atakuwa bibi mkuu wa Mfalme Daudi, na kwa hiyo babu yake Yesu Masihi!
Hbari yao inatukumbusha kwamba mahusiano ya kizazi na kizazi, mahusiano ya maisha na maisha yana faida pande zote mbili. Hakika yunahitajiana! Uanafunzi wa maisha kwa maisha ni kwamba, kila mtu anachangia maisha na mwingine- "kuishi pamoja." Kama yunavyoona katika habari hii ya Naomi na Ruthu, uhusiano kama huo unaweza kutokea hata katika familia zetu!
Kuhusu Mpango huu
![Iron Sharpens Iron: Life-to-Life® Mentoring in the Old Testament](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F23762%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Unatamani "kufanya wanafunzi wanaofanya wanafunzi," kufuatana na Yesu katika Agizo Kuu (Mathayo 28:18-20)? Kama ndivyo, yawezekana umeona kwamba inaweza kuwa vigumu kupata watu wa mfano katika mchakato huu. Utafuata mfano gani? Je, kufanya wanafunzi inaonekanaje katika maisha ya kila siku? Hebu tuangalie katika Agano la Kale jinsi watu watano waume kwa wake walivyowekeza kwa wengine, Life-to-Life®.
More