Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Chuma Hunoa Chuma: Life-to-Life® Mentoring in the Old TestamentMfano

Iron Sharpens Iron: Life-to-Life® Mentoring in the Old Testament

SIKU 2 YA 5

Siku 2: Musa na Yoshua

Musa alikuwa mtu wa Mungu kwa wakati muafaka katika historia ya watu wa Mungu. Mungu alimtumia kuwaongoza Waebrania kutoka Misri na hatimaye kwenye kizingiti cha nchi ya ahadi.

Musa alichagua watu kumi na wawili, kuwakilisha makabila 12 ya Israeli, kuipeleleza nchi. Kati yao alikuwa Yoshua, mwana wa Nuni, kutoka katika kabila la Efraimu (Hesabu 13:16). Yeye, pamoja na mmoja kati ya wale kumi na wawili, Kalebu, walileta habari njema ikionesha ujasiri kwamba, kwa msaada wa Mungu, wangeweza kuimiliki nchi ya ahadi!

Uhusiano wa Musa na Yoshua kwenye vitabu vyote vya Kutoka na Hesabu kunatoa mwanga juu ya umuhimu wa mafunzo ya mtu na mtu katika vizazi vyote. (Kwa ufahamu zaidi, tazama Kutoka 24:13; 32:17; 33:11; na Hesabu 11:25-29; 13:1-14:10.) 

Katika miaka yote 40 ya Waebrania kutembea jangwa la Sinai, Bwana alimtumia Musa kujegwa kuwa mtu "MNENE", mtu ambaye niMwaminiful, Tayari, na Wakufundishika. Kwa kufanya hivyo, katika mafunzo ya mtu na mtu, Musa alimtayarisha kiongozi ajaye wa Waebrania. Yoshua hatimaye angeweza kuwaongoza watu wa Mungu katika nchi ya ahadi.

Tunaweza kujifunza nini katika mfano wa Musa? Kwa maombi ukizingatia kijana katika mzunguko wa ushawishi wako. Kama Mungu alivyomuonesha Musa mtu ambaye alikuwa karibu na Mungu na yeye, yawezekana Mungu akakuonesha mtu "MNENE" kama huyo. Wanaume na wanawake wa Mungu kesho ni akina nani? Yawezekana Mungu atakutumia wewe kuinua viongozi wa baadaye wa familia, marafiki, hata wenye huduma kwa kanisa!

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Iron Sharpens Iron: Life-to-Life® Mentoring in the Old Testament

Unatamani "kufanya wanafunzi wanaofanya wanafunzi," kufuatana na Yesu katika Agizo Kuu (Mathayo 28:18-20)? Kama ndivyo, yawezekana umeona kwamba inaweza kuwa vigumu kupata watu wa mfano katika mchakato huu. Utafuata mfano gani? Je, kufanya wanafunzi inaonekanaje katika maisha ya kila siku? Hebu tuangalie katika Agano la Kale jinsi watu watano waume kwa wake walivyowekeza kwa wengine, Life-to-Life®.

More

Tunapenda kuwashukuru The Navigators kwa kutupa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: https://www.navigators.org/youversion