Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 4 YA 31

Wachungaji walikaa kondeni wakichunga kundi lao usiku wa baridinya Bethlehemu wakiota moto ambao ulikuwa unatoa mwanga kidogo na kuleta joto kidogo. Wachungaji walikuwa watu ambao hawajaelimika, watu wa chini katika jamii wakiwa na masizi vichwani mwao na vinyesinvya kondoo kwenye miguu yao. Wachungaji hawakuwa na matumaini yoyote ya maendeleo... wala matumaini yanwao kumiliki ardhi... wala matumaini ya kupanda kimaisha. Ulimwengu wao haukuwa unabadilika... usiku kwa usiku wa kuchunga kondoo na kuaibishwa kwa dhihaka walizokuwa wanathihakiana katika kuota moto. Ulimwengu wao ulijikita katika kutokukaa sehemu moja, kunung'unika, kuto kutii na kondoo waliojaa kupe. Na wewe unadhani maisha yako ni mabaya?

Usiku mmoja wakiwa wanatetemeka kwa baridi na kujaribu kukaa macho , mbingu zilifunguka katika ulimwengu wao mdogo wenye giza. Wimbo wa malaika ulisikika katika eneo lao na rangi za utukufu kutoka mbinguni zikafunguka, na kundi la malaika likaimba kwa utukufu wimbo mkuu ambao unasikika mpaka leo.

"Tazama, nawaletea habari njema za furaha kuu ambayo itakuwa kwa watu wote!"

Yesu aliuvamia ulimwengu wetu na furaha na bado ni zawadi yake kwako hata leo. Uwepo wake katika maisha yako unafanya giza liondoke na kuzaa tumaini.

Neno la kwanza lililotumika kuelezea kuzaliwa kwa Yesu lilikuwa ni neno "furaha"! Naamini inatakiwa liwe ni neno la kwanza la kukuelezea pia wewe. Furaha ni alama ya kuzaliwa ya mkristo na inatakiwa itulize kila hisia za kupoa kiroho mwilini mwako. Umepigwa chapa ya furaha ya mbinguni na sasa ni zamu yako kuimba wimbo wa malaika!

Maisha yako yanatakiwa yabebe uwepo wa Kristo kwa ulimwengu wenye giza na usio na tumaini. Mariamu alikuwa wa kwanza kumbeba mtoto Yesu ili kwamba na sisi pia, tubebe vinasaba vya kimungu ndani yetu. Vinasaba vya mbinguni vinaitwa "Fu-ra-ha" na ulimwengu wa giza tunaoishi unatamani kuwa nayo!

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com