Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano
Hapa Ayubu anatoa kiapo cha uadilifu. Ingawa kuna kuingizwa majaribuni, haipaswi kukata tamaa. Mtu wa imani huamini hadi anapotoweka (m.6,Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha; Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai). Anajua uzima wa mtu unatokana na Mungu. Amefikia mwisho, pumzi ya Mungu inapoondolewa. Basi, ilimradi anaishi, aendelee kumtegemea atoaye uhai. Ukweli huu Ayubu ataka kuwafundisha waovu wanaomtakia mwaminifu maangamizi. Hawana haki, wala la kujivunia (m.8,Kwani tumaini la mpotovu ni nini, ingawa ajipatia faida, Hapo Mungu amwondoleapo roho yake?). Wakiondokewa na uhai, ni mwisho. Hawana amani. Wanatumani lisilokuwepo (ling. Lk 12:20,Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz