Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 27:1-12

Ayu 27:1-12 SUV

Kisha Ayubu akaendelea na mithali yake, na kusema, Kama aishivyo Mungu, aliyeniondolea haki yangu; Huyo Mwenyezi aliyeitesa nafsi yangu; (Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu, Na roho ya Mungu i katika pua yangu;) Hakika midomo yangu haitanena yasiyo haki, Wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu. Hasha! Nisiwahesabie ninyi kuwa na haki; Hata nitakapokufa sitajiondolea uelekevu wangu. Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha; Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai. Adui yangu na awe kama huyo mwovu, Na mwenye kuondoka kinyume changu na awe kama asiye haki. Kwani tumaini la mpotovu ni nini, ingawa ajipatia faida, Hapo Mungu amwondoleapo roho yake? Je! Mungu atakisikia kilio chake, Taabu zitakapomfikilia? Je! Atajifurahisha katika Mwenyezi, Na kumlingana Mungu nyakati zote? Nitawafundisha ninyi mambo ya mkono wa Mungu; Hayo yaliyo kwa Mwenyezi sitayaficha. Tazama, ninyi nyote mmeyaona wenyewe; Mbona basi mmebatilika kabisa?