Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano
Ayubu anatetea majibu yake kuhusu ukuu na mamlaka ya Mungu. Kwa namna hii anaipambanua imani wazi. Pamoja na mazingira aliyomo, anaona kuwa uweza wa Mungu unatawala, unaongoza, unadhibiti na unatikisa vyote ambavyo mwanadamu anaviogopa. Hivi ni pamoja na kaburi, uovu, nyoka, na maji mengi. Uweza wa Mungu unajionesha pale alipoweka mvua mawinguni, mipaka ya maji na kuitetemesha bahari. Ameupamba uumbaji wake. Hakuna anayeweza kulinganishwa naye Mungu. Je, ni nani kama yeye? Tafakari m.14, Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong'ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuelewa nazo?.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz