Tumaini Linaloishi: Hesabu kuelekea PasakaMfano
“Nifuate.”
Petro alikaa katika huzuni na giza, siku zake zikifuatiwa na kimya cha Mungu. Alikuwa kishamkana Yesu waziwazi kabla hajachukuliwa kwenda kusulubiwa. Na sasa kwa siku chache zilizopita, Petro ilimpasa kubaki katika huzuni na hatia pasipo kutarajia kwamba maumivu yatakoma.
Lakini mapema asubuhi siku ya tatu, kaburi la Yesu lilikutwa tupu na jiwe limeviringishwa pembeni. Wakati Petro na wanafunzi wengine wakiharakisha- wakijaribu kuona matukio ya siku- ghafla Yesu anamtokea Petro akiwa mzima kabisa!
Badala ya kumwacha Petro aishi na aibu ya makosa yaliyopita, Yesu anamvuta pembeni na kumuuliza swali linalompeleka Petro katika kusudi lake:
“Je unanipenda?”
Kwa swali hili, Yesu anamkaribisha Petro kuthibitisha uhusiano alioukana. Nguvu ya Yesu dhidi ya kifo na kuzimu ilimaanisha Petro hastahili kuendelea kubaki kielelezo cha makosa yaliyopita. Angeweza kukubali wito katika maisha yake na kuwa kiongozi ambaye Yesu alijua angekuwa.
Kama Petro, una nafasi ya kusema "ndiyo" kumpenda Yesu na kupendwa na Yeye. Haijalishi maisha yako yanaonekana ni ya hovyo kiasi gani, au unajisikia kuwa mbali na Yesu kiasi gani, hakuna kinachoweza kukutenga na upendo wake. Makosa yako ya zamani au matatizo yako ya sasa hayaelezi kusudi lako maisha yako yanapokuwa na mizizi katika Kristo pekee.
Ufufuo unatuhakikishia kwamba hakuna hali au makosa ya kumfanya Mungu asiokoe. Hakuna hofu ambayo Yesu hawezi kuishinda na hakuna maisha asiyoweza kuyaponya. Hakuna giza linaloweza kusimama kinyume na nguvu ya Mungu aliyefufuka aliyeshinda mauti kwa niaba yetu. Hakuna kitu Mungu wetu hawezi kufanya.
Omba: Yesu, asante kwa kushinda mauti kwa ajili yangu. Nakushukuru kwa sababu hakuna kinachoweza kunitenga na upendo wako, na hakuna makosa yanayoweza kunikosesha sifa katika mipango yako. Leo, nikumbushe kwamba umeniita niwe mtu wa namna gani. Na ninapoanza kujisikia sistahili, nisaidie kukumbuka kutazama kufufuka kwako na kufurahi kwamba wewe pekee ndiyo wokovu wangu. Ninakupenda, na leo nachagua kukufuata.
Kuhusu Mpango huu
Giza linapokuzunguka, ulikabili namna gani? Kwa siku 3 zijazo, zama katika hadithi ya Pasaka na ugundue jinsi ya kushikilia tumaini pale unapojisikia kuachwa, mpweke au usiye wa thamani.
More