Tumaini Linaloishi: Hesabu kuelekea PasakaMfano
"Kwa nini Umeniacha?"
Fikiria unamtazama Yesu akiwa msalabani. Njia pekee anayoweza kupumua ni kwa kujivuta dhidi ya misumari katika mikono na vifundo vya miguu Yake.
Kama tukiwa wakweli, kuna uwezekano sisi sote tumepitia nyakati ambapo tulimuuliza Mungu, "Uko wapi katika hili? Kwa nini umeniacha?"
Ni namna gani tunajibu tunapojikuta katika hali ya kuwa peke yetu, wenye wasiwasi, au tulioachwa?
Maneno aliyozungumza Yesu msalabani ni dhahiri yamechukuliwa kutoka Zaburi 22—ombolezo la kinabii lililoandikwa na Mfalme Daudi. Katika namna nyingi, Zaburi hii inamhusu Yesu, lakini pia inatupatia hatua tatu za kufuata tunapojihisi wapweke:
1. Kuwa muwazi kwa Mungu juu ya hisia zako.
/Mahusiano huanza na kuwa halisi. Kwa hiyo kama unahisi umeachwa na Mungu, mwambie hivyo. Muulize Mungu maswali yako, na uuandae moyo wako kusikia majibu yake.
2. Hata hivyo mpe Mungu utukufu.
Hisia zetu hazibadili ukweli kwamba Mungu anastahili kuabudiwa. Kwa kweli, mara nyingi kupitia kuabudu ndipo tunapogundua tiba ya wasiwasi wetu. Tunapojikita katika Mungu ni nani, mtazamo wetu mwishowe hubadilika—hata kama hali yetu isipobadilika.
3. Mkumbushe Mungu ahadi zake.
Katika Zaburi yote ya 22, ni dhahiri kwamba Daudi anamwambia Mungu, "Najua Wewe ni nani. Na kwa kuwa umkweli, niokoe mimi kama ulivyowaokoa watu Wako kabla yangu." Kumkumbusha Mungu juu ya ahadi Zake sio tu ni tendo la imani, bali pia inatusaidia kukumbuka uaminifu wa Mungu.
Mwishowe, uaminifu wa Mungu ulidhihirishwa pale Yesu aliposulubiwa. Yesu kwa hiari yake aliteseka msalabani ili tuweze kuufurahia urafiki wa milele na Mungu. Yesu ni timilizo la unabii wa Zaburi ya 22. Na, kwa sababu Yeye alistahimili kutengwa na Mungu, hatuna haja ya kutengwa tena.
Tumia wakati kidogo kuwaza juu ya sadaka kuu ya Yesu kwa ajili yako.
Omba:Yesu, asante kwa kunikomboa kutoka katika kutengwa nawe milele. Ni kwa sababu ulistahimili kutengwa na Baba Yako kwa hiari ili mimi nisiwe na haja hiyo. Leo, nisaidie nitulie na niwaze juu ya ukuu wa sadaka Yako, na nikurudishie Wewe utukufu unaostahili kwa haki. Haijalishi hisia zangu, daima Wewe unastahili kuabudiwa. Kwa hiyo leo, nachagua kukuabudu Wewe. Katika jina la Yesu, Amina.
Kuhusu Mpango huu
Giza linapokuzunguka, ulikabili namna gani? Kwa siku 3 zijazo, zama katika hadithi ya Pasaka na ugundue jinsi ya kushikilia tumaini pale unapojisikia kuachwa, mpweke au usiye wa thamani.
More