Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano
Vita vile vilikuwa vikali sana siku ile; naye Abneri akashindwa, na watu wa Israeli, mbele ya watumishi wa Daudi (m.17). Makabila mengine nje ya Yuda kwa pamoja yaliitwa "Israeli". Sasa imeanza vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ndugu hupigana na ndugu (katika m.26 Abneri anamwuliza Yoabu, Itakuwa hata lini usijewaamuru watu warudi na kuacha kuwafuatia ndugu zao?). Wenye ushindi siku ile ni jeshi la Daudi. Na wao ndio waliozidi kuwa na nguvu siku hadi siku. Ila Ishboshethi na Abneri na watu wao walizidi kupungua nguvu. Basi kulikuwa na vita siku nyingi kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi; Daudi akaendelea akasitawi, lakini nyumba ya Sauli ikaendelea kudhoofika(3:1). Hii ni kwa sababu Mungu alikwisha mchagua Daudi awe mfalme wa watu wake badala ya Sauli.Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe (1 Sam 16:1; ukitaka kujua zaidi, soma 1 Sam 15:26-28 na 16:11-13).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz