Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

SIKU 2 YA 31

Daudi kumwombolezea Sauli ni jambo la pekee. Katika baadhi ya zaburi zake, Daudi anamwomba Mungu awaangamize adui zake. Mfano mmoja ni Zaburi 59:12-13 inayomhusu watumishi wa Sauli wakati alipomtafuta Daudi ili kumwua: Kwa dhambi ya kinywa chao, Na kwa neno la midomo yao, Wanaswe kwa kiburi chao, Kwa ajili ya kulaani na uongo wasemao. Uwakomeshe kwa hasira, Uwakomeshe watoweke, Wajue ya kuwa Mungu atawala katika Yakobo, Na hata miisho ya dunia. Hata hivyo Daudi hakujilipiza kisasi mwenyewe. Alimwachia Mungu kulipa kisasi! Daudi akasema, Aishivyo Bwana, Bwana atampiga; au siku yake ya kufa itampata; atashuka kwenda vitani na kupotea. Hasha! Nisiunyoshe mkono wangu juu ya masihi(1 Sam 26:10-11). Yesu Kristo ametuonyesha huruma iliyo kubwa zaidi. Hata hili la kumwomba Munguatulipize kisasi adui zetu amekataa! Aliwaombea mema waliomwudhi! Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo(Luka 23:34). Warumi 12:18-21 hutuonyesha jinsi ya kufanya: Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz