Kutafuta Njia ya Kumrudia MunguMfano
"Siwezi Fanya Haya Peke Yangu"
Bila kujali tulipo katika safari yetu ya kumurudia Mungu, sisi wote tuko na mambo maishani mwetu ambayo bado tunayashikilia. Kwa wengine, ni shughuli ya siri au tabia ambayo hakuna anayeijua. Na wengine, ni dhahiri kabisa nini tunachotafuta.
Ni nini kwako? Ni nini unachohitaji kuachilia? Ni nadra sana kwa Mungu kuweka kitu kipya maishani mwako hadi uachilie kitu kizee au kilichofunjika maishani.
Ndio maana hatua ya pili baada ya muamko kwa majuto ni muamuko wa kusaidiwa. Huu muamko wa tatu ni hatua kubwa sana kuelekea karibu na Mungu kwa sababu tunagundua hatuwezi fanya peke yetu. Nini kinachotokea baadaye?
Tunapiga simu.
Tunakuwa na hayo mazungumzo.
Tanaenda kwa kikundi cha msaada.
tunajipata tukiporomoka katika safu ya nyuma kanisani
Tunapiga magoti na kumlilia Mungu, "Mungu kama wewe ni wa kweli . . . !"
Kuyapa kisogo chaguo haribifu na kutafuta msaada ni sehemu ya toba. Kutubu ni kwenda nyumbani, kurejea kule ulikotoka na kule ambapo unamilikiwa. Kwenda nyumbani ni kusamehewa na kupokea uhakika wa maisha baada ya maisha haya, lakini pia ni kuhusu kupata maana mpya na muelekeo wa maisha ambayo huwezi pata mahali pengine. Ni kuhusu kuwa na uhusiano na Mungu. Ni kuhusu kuelekeza tena maisha yako na kurudi kule umetoka na kule unamilikiwa. Unapotubu, Mungu hukubadilisha. Unakuwa mtu tofauti. Biblia inasema kuwa Roho wa Mungu huja kuishi ndani yako, na matokeo yake ni mageuzi ya kutambulika na yanayoendelea.
Weka akilini kuwa kutubu hakumaanishi kuhisi vibaya. Kama jambo la kweli, Biblia husema toba ya kweli hutuelekeza kwa "muda wa kuonyesha upya" kutoka kwa Mungu. Toba ni kuhusu kuanza upya na kukiri, "Nahitaji usaidizi." Wito huu wa kutubu, kuachana na dhambi zetu na kurudi nyumbani kwa Mungu, ni kwa kila mtu.
Hii inaweza kuwa siku ambayo unaenda nyumbani. Simama hapo ulipo na uje nyumbani kule ulikotoka. Haijalishi ni maamuzi yepi mabaya umefanya siku za kale au hapo mbeleni. Mungu anakuambia, "Chochote ulichokifanya, chochote kile umekua, haijalishi. Njoo nyumbani tu."
Ni nini unahitaji kutubu leo? Ni jinsi gani kutubu kutakuelekeza kwa "muda wa kuonyesha upya" na Mungu?

Andiko
Kuhusu Mpango huu
Je, unatafuta mengi kutoka kwa maisha? Kutaka mengi ni kuwa na hamu ya kumrudia Mungu— popote uhusiano wako na Mungu upo sasa. Sisi sote hushuhudia ishara—au muamko—tunapotafuta kumrudia Mungu. Safari kupitia kwa moja wepo ya miamko hizi na kupunguza umbali kati ya ulipo sasa na wapi unataka kuwa. Tunataka kumpata Mungu, anataka hata mengi yapatikane..
More
Tungependa kuwashukuru Dave Ferguson, Jon Ferguson na Kikundi cha uchapishaji cha WaterBrook Multnomah kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://waterbrookmultnomah.com/catalog.php?work=235828