Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutafuta Njia ya Kumrudia MunguMfano

Finding Your Way Back To God

SIKU 1 YA 5

"Inatakiwa kuwa na mengi"

Je, huwa una hisi kuwa unatafuta kitu maishani ambacho hakitakukidhi kikamilifu? Usipuzilie mbali hisia hiyo. Ni kutoka kwake Mungu.

Hatuzungumzii kuhusu madawa ya kulevya, ingawaje kunya pombe ni njia hakika za kutafuta vitu bure. Lakini tumewajua "watu wazuri wa kanisani" ambao huketi kanisani kila wiki—au wanaohubiri katika mimbari kwa watu hao—ambao wanajihisi kuwa mbali na Mungu, "Wamefanikiwa" au "wako pamoja" au "wenye haki" kwa nje, lakini wanamkosa Mungu kwa undani. Wanajishughulisha na mambo na kazi za kidini, shule, au familia, lakini Wanatamani Mungu awahisi.

Hiyo hali ya kumtaka Mungu ni muamko wa kiroho wa kwanza kwa sisi wote ambao tunatafuta njia ya kumrudia Mungu. "Kuna zaidi ya hayo."

Unapotamani upendo ambao ni wa kina na unaotosheleza, unapotaka kujipatia kwa kitu ambacho kitaleta mabadiliko ya ukweli, au unapotafuta majibu ya maswali magumu ya maisha, unamtafuta Mungu. Una chaguo mbili: unaweza endelea kutafuta ili kujitosheleza kwa njia zako mwenyewe, au unaweza kumtazamia Yule ambaye alikupatia hizo hisia za kutamani kutoka mwanzo.

Hamu yetu ya upendo wa ukweli inaturudisha hadi jinsi mwanadamu alivyoumbwa hapo mwanzo. Mungu alikusudia kwamba tushuhudie upendo wake moja kwa moja kutoka kwake na kupitia wengine tunaohusiana nao kwa njia nzuri. Kile tunachohamu nacho, sio tu Mungu anacho bali pia Mungu ni hicho kitu. Yeye ni upendo na anatufuata na upendo.

Tumeyasikia yakisemwa kuwa kila anayebisha mlango wa danguro anamtafuta Mungu. Ikiwa unabisha mlango wa tabia na husiano za kibinafsi na za uharibifu, unaweza kuwa umefika hatua muhimu katika safari yako ya kumrudia Mungu. Kwa nini? Kwa sababu masikitiko utakayo kuwa nayo kwa kuchagua vitu nafuu mbadala yatakufanya uanze kuwaza ni wapi utapata upendo wa kweli. Je, utamuacha Mungu ajaze hamu yako ya kupenda na kupendwda?

Ni nini shughuli zako za wiki hii zanaashiria kuhusu unachofikiria kitakutosheleza?
siku 2

Kuhusu Mpango huu

Finding Your Way Back To God

Je, unatafuta mengi kutoka kwa maisha? Kutaka mengi ni kuwa na hamu ya kumrudia Mungu— popote uhusiano wako na Mungu upo sasa. Sisi sote hushuhudia ishara—au muamko—tunapotafuta kumrudia Mungu. Safari kupitia kwa moja wepo ya miamko hizi na kupunguza umbali kati ya ulipo sasa na wapi unataka kuwa. Tunataka kumpata Mungu, anataka hata mengi yapatikane..

More

Tungependa kuwashukuru Dave Ferguson, Jon Ferguson na Kikundi cha uchapishaji cha WaterBrook Multnomah kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://waterbrookmultnomah.com/catalog.php?work=235828