Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Usijisumbue kwa LoloteMfano

Anxious For Nothing

SIKU 7 YA 7

Yawezekana moja ya hadithi hizo imekugusa. Au yawezekana hadithi yako kuhusu hofu ni ya tofauti kabisa. Lakini vita yoyote unayokabiliana nayo hofu, Roho yule yule aliyemfufua Kristo kutoka kwa wafu anaishi ndani yako. Na hakukupa Roho ya hofu.

Hiyo haimaanishi kama unashindana na hofu huna imani ya kutosha. Haimaanishi humwamini Mungu vyakutosha. Ukweli ni, je itakuwaje kama hofu ndiyo kitu kitakachokusaidia kujifunza kumtegemea na kumwamini Mungu? Yawezekana hofu yaweza kuwa ndiyo kichocheo cha kumkaribia Mungu?

Hofu inakuwa ni zawadi inapotusaidia kumtegemea Mungu. Haimaanishi tuache kuomba msaada au kutumaini. Ina maana kwamba tunajua kutafuta amani ni hatua.

Kwa hiyo, yawezekana kutosumbukia chochote? Ndiyo. Hiyo haimaanishi kwamba hakutakuwa na chochote cha kuogopa. Lakini kwa sababu ya Yesu, tunaweza tusimbukie chochote hata kama kuna kitu cha kusumbukia--si kwa juhudi zetu wenyewe bali kwa uwepo wake. Angalia mistari hii tena:

Msijisumbue kwa neno lolote, bali kwa kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. Wafilipi 4:6-7 SUV 

Ishi katika kweli hiyo. Mara nyingi tunashikilia neno "amani," lakini linasema, " amani ya Mungu.” Amani ya kweli inapatikana tuu katika uwepo wa Mungu. Kwa hiyo itakuwaje kama jibu la hofu siyo kutokuwa na msongo bali Mungu zaidi?

Tafakari: Ninawezaje mara kwa mara kukaribisha uwepo na amani ya Mungu katika maisha yangu? 

Omba: Bwana, asante kwa uwepo wako. Ninakuja kwako leo naomba amani utowayo. Nakuhitaji zaidi. Nakukaribisha katika kila eneo la maisha yangu. Nisaidie kukutegemea zaidi na kikamilifu leo. Ninakupa hofu yangu yote na mashaka. Nisaidie kutokusumbukia chochote kwa kukutegemea. Nakutumaini. Najitoa kwako. Katika jina la Yesu, amen.  

Kama unapambana na hofu, au mtu unayempenda, kuna msaada na tumaini.Jifunze zaidi kuhusu namna ambavyo hofu inaweza kuonekana, unavyoweza kushughulika nayo, na jinsi ya kuwasaidia wengine wanaopambana nayo..

siku 6

Kuhusu Mpango huu

Anxious For Nothing

Ingekuwaje kama kungekuwa na njia bora ya kupigana na hofu isiyoisha inayokufanya kukosa usingizi? Pumziko halisi lipo--yawekana karibu zaidi ya unavyofikiria. Badilisha hofu na amani kupitia siku hizi 7 za mpango wa Biblia kutoka Life.Church, ikiambatana na mfululizo wa ujumbe wa Mchungaji Craig Groeschel Usijisumbue kwa Lolote.

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/