Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Usijisumbue kwa LoloteMfano

Anxious For Nothing

SIKU 3 YA 7

Je amani inawezekana leo? Cheri alifanya jitihada miaka 11 iliyopita kutafuta ukweli. Hiki ndicho alichokigundua njiani: 

Ninakumbuka wazi wazi. Siku niliyoamua siwezi kuishi hivi tena.

Haya, mfuasi halisi wa Kristo, nikiyakabili maisha kama wengine. Niliishia katika mashaka na hofu, lakini nikijua haitakiwi kuwa hivyo! Mara kwa mara nilisoma katika neno la Mungu kutokuogopa na kutojisumbua kwa lolote. Lakini hiyo ilionekana haiwezekani!

Mungu ana mengi ya kusema katika Biblia juu ya hofu na dawa yake: amani. Wakati fulani, Yesu na wanafunzi wake walikuwa katika chombo wakivuka bahari ya Galilaya wakati dhoruba kali ilitishia kuwazamisha. Wote walijitahidi wasiangamie, na Yesu alikuwa anafanya nini? Alikuwa amelala! Katika ya dhoruba.

Wanafunzi wake wakamuuliza, "Mwalimu, huoni kwamba tunazama?" Yesu aliamka na kukemea dhoruba, na ikatulia. Ndipo akawauliza wanafunzi, " mbona mmekuwa waoga? hamna imani bado? Marko 4:40 SUV

Hicho kilihitimisha mazungumzo niliyokuwa nayo na Mungu. Niliweza kumhisi akiniuliza kwa nini nilikuwa naogopa, na nilikuwa namjibu, Si ni sawa? Angalia mazingira yangu! Ni nani ambaye asingeogopa

Katika kutafuta amani kwangu, mambo mengi yalikuwa dhahiri.

  1. Mazingira yangu yalikuwa yanaamua kiwango cha amani yangu.. Kama mazingira ya maisha yangu yangekuwa yote mema, basi ningekuwa na amani. Kama dhoruba ilikuwa inanizunguka, nilikuwa katika msongo wa mawazo, hofu na kuchoka wakati wote--kuchoshwa na hisia zangu. Nilikuwa kama wanafunzi katika dhoruba. Niliogopa dhoruba, niliumia, na kuchanganyikiwa kwa sababu nilifikiria Mungu hakujali. Lakini Yesu alinileta katika hatua ya pili.
  2. Yesu alikuwa anajaribu kunifundisha amani kama inawezekana, pasipokujali dhoruba. . Unafananisha na vita hii? Siyo rahisi, siyo? Nilikuwa bado najitahidi kuelewa namna gani Yesu alitarajia mimi kupata amani katika dhoruba, nikijiuliza kama kweli alijali, nilipopata mpenyo wangu wa pili. 
  3. Dhoruba ilionyesha kiwango changu cha imani. Amani haimaanishi kila kitu kinaenda sawa katika maisha yako. Ina maana kuwa na amani wakati wa dhoruba inatikisa maisha yako. Sikujifunza kumtumaini Mungu na kuwa na amani hata katika dhoruba hizo. Umegonga ukuta huyo tayari?

Ni wazi nilikuwa na nafasi ya kukua. Lakini ninajifunza kwamba njia ya amani inapatikana kwa kumtumaini na kuweka mawazo yako kwa ambaye hasumbuliwi na dhoruba. Haikutokea ghafla, lakini taratibu, amani zaidi na utulivu vilihuisha uchovu wangu, nafsi iliyochoka. 

-Cheri  

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Anxious For Nothing

Ingekuwaje kama kungekuwa na njia bora ya kupigana na hofu isiyoisha inayokufanya kukosa usingizi? Pumziko halisi lipo--yawekana karibu zaidi ya unavyofikiria. Badilisha hofu na amani kupitia siku hizi 7 za mpango wa Biblia kutoka Life.Church, ikiambatana na mfululizo wa ujumbe wa Mchungaji Craig Groeschel Usijisumbue kwa Lolote.

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/