INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SABAMfano

YESU ATEMBEA JUU YA MAJI
22 Mara Yesu akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye chombo watangulie kwenda ng'ambo ya pili ya bahari, wakati yeye anawaaga wale makutano.
23 Baada ya kuwaaga, akaenda zake mlimani peke yake kuomba. Jioni ilipofika, Yesu alikuwa huko peke yake.
24 Wakati huo kile chombo kilikuwa kimeshafika mbali kutoka nchi kavu kikisukwasukwa
na mawimbi kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho.
"25 Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Yesu akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji.
26 Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu, wakasema,"
“Ni mzimu.” Wakapiga yowe kwa kuogopa.Lakini mara Yesu akasema nao, akawaambia,
“Jipeni moyo! Ni Mimi. Msiogope.”
28 Petro akamjibu, “Bwana, ikiwa ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji.”
Yesu akamwambia, “Njoo.” Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Yesu.
30 Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, huku akipiga kelele,
“Bwana, niokoe!”
31 Mara Yesu akanyosha mkono wake na kumshika, akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini uliona shaka?”
32 Nao walipoingia ndani ya chombo, upepo ukakoma.Ndipo wote waliokuwamo ndani ya kile chombo wakamwabudu Yesu wakisema,
“Hakika, wewe ndiwe Mwana wa Mungu.”
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More
Tunapenda kushukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org