INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SABAMfano

YESU AWATUMA WANAFUNZI KUMI NA WAWILI
7 Akawaita wale kumi na wawili, akawatuma wawili wawili na kuwapa mamlaka kutoa pepo wachafu.
Akawaagiza akisema, “Msichukue cho chote kwa ajili ya safari isipokuwa fimbo tu. Msichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kwenye mikanda yenu, bali mvae viatu, lakini msivae nguo ya ziada.”
10 Akawaambia, “Mkiingia kwenye nyumba yo yote, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo.Kama mahali po pote hawatawakaribisha wala kuwasikiliza,mtakapoondoka huko,
kung'uteni mavumbi yaliyoko miguuni mwenu, ili kuwa ushuhuda dhidi yao.”
12 Kwa hiyo wakatoka na kuhubiri kwamba inawapasa watu kutubu na kuacha dhambi.
13 Wakatoa pepo wachafu wengi, wakawapaka wagonjwa wengi mafuta na kuwaponya.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More
Tunapenda kushukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org