INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA NANEMfano
KUREJESHA UHUSIANO WA KIKRISTO
15 “Kama ndugu yako akikukosea, nenda ukamwonyeshe Kosa Lake, kati yenu ninyi wawili peke yenu. Kama akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako.
16 Lakini kama hatakusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili ili kila neno lithibitishwe na ushahidi wa mashahidi wawili au watatu.
17 Kama akikataa kuwasikiliza hao, liambie kanisa, naye kama akikataa hata kulisikiliza kanisa, basi mtendeeni mtu huyo kama vile ambavyo mngemtendea asiyeamini.
“Amin, nawaambia, lo lote mtakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni na lo lote mtakalolifungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.“Tena nawaambia, ikiwa wawili wenu watakubaliana duniani kuhusu jambo lo lote watakaloomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni."
20 Kwa kuwa wanapokusanyika pamoja watu wawili au watatu kwa Jina langu, mimi niko papo hapo pamoja nao.” Ndipo Petro akamjia Yesu na kumwuliza,
“Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Je, hata mara saba?”
Yesu akamjibu, “Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More
Tunapenda kushukuru GNPI-Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org