INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILIMfano
![INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILI](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F15962%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
YESU AMWONEKANIA MARIAMU MAGDALINI
"10 Kisha hao wanafunzi wakaondoka wakarudi nyumbani kwao. Lakini Maria Magdalene akasimama nje ya kaburi akilia. Alipokuwa akilia, akainama, kuchungulia mle kaburini,
"12 naye akaona malaika wawili wamevaa mavazi meupe, wameketi pale mwili wa Yesu ulipokuwa umelazwa, mmoja upande wa kichwani na mwingine upande wa miguuni. Wakamwuliza Maria,
“Mwanamke, mbona unalia?” Akawaambia,
“Nalia kwa kuwa wamemchukua Bwana wangu na sijui walikomweka.”
14 Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Yesu amesimama, lakini hakumtambua.
15 Yesu akamwambia, “Mwanamke, mbona unalia? Unamtafuta nani?”
Maria akidhani ya kuwa aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akamwambia,
“Bwana, kama ni wewe umemchukua, tafadhali nionyeshe ulikomweka, nami nitamchukua.”
16 Yesu akamwita,
“Maria!” Ndipo Maria akamgeukia Yesu na kusema naye kwa Kiebrania,
“Rabboni!” "(Maana yake Mwalimu).
17 Yesu akamwambia,
“Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ ”
18 Kwa hiyo Maria Magdalene akaenda kuwatangazia wanafunzi wa Yesu akisema,
“Nimemwona Bwana!” "Naye akawaambia kwamba amemweleza mambo hayo yote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILI](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F15962%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More
Tunapenda kushukuru GNPI-Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org