Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILIMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILI

SIKU 4 YA 7

KUSULUBISHWA NA KUZIKWA KWA YESU

LUKE 23:26-32

26 Walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja aitwaye Simoni mwenyeji wa Kirene, aliyekuwa anatoka shambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha auchukue nyuma ya Yesu.

"27 Idadi kubwa ya watu wakamfuata Yesu, wakiwamo wanawake waliokuwa wakimlilia na kumwombolezea.

28 Yesu akawageukia, akawaambia, “Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi bali jililieni ninyi wenyewe na watoto wenu.

29 Kwa maana wakati utafika mtakaposema, ‘Wamebarikiwa wanawake tasa, ambao matumbo yao hayakuzaa, wala matiti yao hayakunyonyesha!’

32 Watu wengine wawili wahalifu, walipelekwa pamoja na Yesu ili wakasulibiwe.

MATTHEW 27

33 Wakafika mahali paitwapo Golgotha (ambayo maana yake ni, Mahali pa Fuvu la Kichwa),

34 wakampa Yesu divai iliyochanganywa na nyongo ili anywe, lakini alipoionja, akakataa kuinywa.

LUKE 23

33 Walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, hapo ndipo walipomsulibisha Yesu pamoja na hao wahalifu, mmoja upande wake wa kuume na mwingine upande wake wa kushoto.

34 Yesu akasema, “Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!”

JOHN 19

23 Askari walipokwisha kumsulibisha Yesu, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini.

24 Wakaambiana, “Tusilichane ila tulipigie kura ili kuamua ni nani alichukue.”

"Hili lilitukia ili Maandiko yapate kutimizwa yale yaliyosema, “Waligawana nguo zangu na mavazi yangu wakayapigia kura.”

MARK 15

25 Ilikuwa yapata saa tatu asubuhi walipomsulibisha.

JOOHN 19

19 Pilato akaamuru tangazo liandikwe na liwekwe juu kwenye msalaba wa Yesu:

“YESU WA NAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI.”

20 Kwa kuwa mahali hapo aliposulibiwa palikuwa karibu na mjini, Wayahudi wengi walisoma maandishi haya yaliyokuwa yameandikwa kwa lugha za Kiebrania, Kiyunani na Kilatini.

21 Viongozi wa makuhani wa Wayahudi wakapinga, wakamwambia Pilato, “Usiandike, ‘Mfalme wa Wayahudi,’ bali andika kwamba, mtu huyu alisema, ‘Mimi ni mfalme wa Wayahudi.’ 

22 Pilato akawajibu, “Nilichokwisha kuandika, nimeandika!”

MARK 15

29 Watu waliokuwa wakipita karibu wakamtukana na kutikisa vichwa vyao kwa mzaha wakisema, 

“Aha! Wewe ambaye ungelibomoa Hekalu na kulijenga kwa siku tatu, basi ujiokoe mwenyewe na ushuke kutoka msalabani.”

31 Vivyo hivyo viongozi wa makuhani pamoja na walimu wa sheria wakamdhihaki miongoni mwao wakisema, 

“Yeye aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe! Basi huyu Kristo, huyu Mfalme wa Wayahudi, ashuke sasa kutoka msalabani, ili tupate kuona na kuamini.”

Wale waliosulibiwa pamoja naye pia wakamtukana.

LUKE 23

39 Mmoja wa wale wahalifu waliosulibiwa pamoja naye akamtukana, akasema: “Wewe si ndiye Kristo? Jiokoe ili utuokoe na sisi.”

40 Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akasema, “Je, wewe humwogopi Mungu, wakati uko kwenye adhabu hiyo hiyo?

41 Sisi tumehukumiwa kwa haki kwa kuwa tunapata tunayostahili kwa ajili ya matendo yetu. Lakini huyu mtu hajafanya kosa lo lote.”

42 Kisha akasema, “Bwana Yesu, unikumbuke utakapokuja katika Ufalme wako.”

43 Yesu akamjibu, “Amin, nakuambia, leo hii utakuwa pamoja nami Paradiso.”

JOHN 19 

31 Kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalio ya Pasaka, Wayahudi hawakutaka miili ibaki msalabani siku ya Sabato, hasa kwa kuwa hiyo Sabato ingekuwa Sikukuu.

Wakamwomba Pilato aamuru miguu ya wale waliosulibiwa ivunjwe ili wafe haraka miili iondolewe kwenye misalaba.

32 Kwa hiyo maaskari wakaenda wakavunja miguu ya mtu wa kwanza aliyesulibiwa pamoja na Yesu na yule mwingine pia.

33 Lakini walipomkaribia Yesu, wakaona ya kuwa amekwisha kufa, hivyo hawakuvunja miguu yake.

34 Badala yake mmoja wa wale maaskari akamchoma mkuki ubavuni na mara pakatoka damu na maji.

"36 Kwa maana mambo haya yalitukia ili Maandiko yapate kutimia, yale yasemayo, “Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.”

37 Tena Maandiko mengine yanasema, “Watamtazama yeye waliyemchoma kwa mkuki.”

MARK 15

33 Ilipofika saa sita, giza lilifunika nchi yote mpaka saa tisa.

34 Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Eloi, Eloi lama Sabakthani?”

Maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”

35 Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama karibu waliposikia maneno hayo, wakasema, “Msikieni anamwita Eliya.”

LUKE 23

46 Yesu akapaza sauti yake akasema, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.

MATTHEW 27

51 Wakati huo huo pazia la Hekalu likachanika vipande viwili, kuanzia juu hadi chini. 

Dunia ikatetemeka na miamba ikapasuka. Makaburi yakafunguka na miili ya watakatifu waliokuwa wamekufa ikafufuka.

53 Wakatoka makaburini na baada ya Yesu kufufuka waliingia kwenye Mji Mtakatifu na kuwatokea watu wengi.

MARK 15

39 Basi yule jemadari, aliyekuwa amesimama hapo mbele ya msalaba wa Yesu, aliposikia ile sauti yake na kuona jinsi alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”

40 Walikuwapo pia wanawake waliokuwa wakiangalia kwa mbali, ambao miongoni mwao alikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo mdogo na Yose, pia na Salome.

41 Hawa walifuatana na Yesu na kumhudumia alipokuwa Galilaya. "

Pia walikuwapo wanawake wengine wengi waliokuwa wamekuja pamoja naye Yerusalemu.

JOHN 19

31 Kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalio ya Pasaka, Wayahudi hawakutaka miili ibaki msalabani siku ya Sabato, hasa kwa kuwa hiyo Sabato ingekuwa Sikukuu.

Wakamwomba Pilato aamuru miguu ya wale waliosulibiwa ivunjwe ili wafe haraka miili iondolewe kwenye misalaba.

32 Kwa hiyo maaskari wakaenda wakavunja miguu ya mtu wa kwanza aliyesulibiwa pamoja na Yesu na yule mwingine pia.

33 Lakini walipomkaribia Yesu, wakaona ya kuwa amekwisha kufa, hivyo hawakuvunja miguu yake.

34 Badala yake mmoja wa wale maaskari akamchoma mkuki ubavuni na mara pakatoka damu na maji.

"36 Kwa maana mambo haya yalitukia ili Maandiko yapate kutimia, yale yasemayo, “Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.”

37 Tena Maandiko mengine yanasema, “Watamtazama yeye waliyemchoma kwa mkuki.”

MARK 15

"42 Ilipofika jioni, kwa kuwa ilikuwa Siku ya Maandalizo, siku moja kabla ya Sabato, Yosefu wa Arimathaya mtu aliyeheshimiwa katika Baraza, ambaye yeye mwenyewe alikuwa anautarajia Ufalme wa Mungu, akamwendea Pilato kwa ujasiri na kumwomba huo mwili wa Yesu.

"44 Pilato alikuwa akijiuliza kama Yesu alikuwa amekwisha kufa. Akamwita yule jemadari, akamwuliza iwapo Yesu alikuwa amekwisha kufa.

45 Baada ya kupata habari kutoka kwa yule jemadari kwamba kweli amekwisha kufa, Pilato akampa Yosefu ruhusa ya kuuchukua huo mwili.

JOHN 19

39 Naye Nikodemo, yule ambaye kwanza alimwendea Yesu usiku, akaja, akaleta mchanganyiko wa manemane na manukato, yenye uzito wa zaidi ya kilo thelathini.

40 Wakauchukua mwili wa Yesu, wakauviringishia sanda ya kitani safi pamoja na yale manukato, kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi.

41 Basi palikuwa na bustani karibu na mahali pale aliposulibiwa, nako ndani ya ile bustani palikuwa na kaburi jipya, ambalo hajazikiwa mtu bado.

42 Kwa hiyo, kwa kuwa ilikuwa siku ya Wayahudi ya Maandalio, nalo kaburi hilo lilikuwa karibu, wakamzika Yesu humo.

LUKE 23

55 Wale wanawake waliokuwa wamekuja pamoja na Yesu wakimfuata kutoka Galilaya, wakamfuata Yosefu, wakaliona kaburi na jinsi mwili wa Yesu ulivyolazwa.

"56 Kisha wakarudi nyumbani, wakaandaa manukato na marhamu ya kuupaka huo mwili. Lakini wakapumzika siku ya Sabato kama ilivyoamriwa.

MATTHEW 27

62 Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile ya Maandalizi ya Sabato, viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakamwendea Pilato

63 na kusema, “Bwana, tumekumbuka kwamba yule mdanganyifu kabla hajafa alisema, ‘Baada ya siku tatu nitafufuka.’

64 Kwa hiyo uamuru kaburi lilindwe kwa uthabiti mpaka baada ya siku tatu. 

La sivyo, wanafunzi wake wanaweza kuja kuuiba mwili wake na kuwaambia watu kwamba amefufuka kutoka kwa wafu. Udanganyifu huu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa kwanza.”

65 Pilato akawaambia, “Ninyi mnao askari walinzi. Nendeni, liwekeeni ulinzi kadri mwezavyo.”

66 Kwa hiyo wakaenda na walinzi ili kulilinda kaburi kwa uthabiti, wakatia muhuri kwenye lile jiwe na kuweka ulinzi.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana

More

Tunapenda kushukuru GNPI-Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org