Uwekezaji Wako Ulio Bora!Mfano
“Tumia Kanuni za Ki-Mungu Kila Siku”
“Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.” Zaburi 119:105
Kwa Wakristo, Neno la Mungu linatoa nguvu ya mwanga katika wakati ambao ni ulimwengu wa giza. Neno la Mungu litakuwa chanzo hicho cha mwanga kama tutakuwa wazi kwa kweli zake na kuliruhusu kuzama ndani ya maisha yetu. Yesu analielezea hili katika mfano unaopatikana katika kitabu cha Mathayo:
“Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda. Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila; nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina; na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka. Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga; nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini.” Mathayo 13:3-8
Mbegu katika hadithi inawakilisha Biblia, na hali tofauti za udongo zinawakilisha utayari na uhiari wetu wa kupokea neno la Mungu. Kumbuka kwamba si mbegu zote zilizopandwa na mkulima zilitoa matokeo aliyoyatarajia, bali ni zile mbegu zilizopandwa kwenye udongo mzuri tu. Soma Mathayo 13:18-23 kuona ufafanuzi wa Yesu wa simulizi hiyo. Kulima katika “udongo mzuri” maishani mwetu ina maana tunaruhusu Neno la Mungu kupenya mawazo yetu na kushawishi shauku na tabia za mioyo yetu.
“Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.” Waebrania 4:12
Kuhusu Mpango huu
Kupata matunda tele na ya baraka huanzia na kufanya uwekezaji ulio sahihi. Kama wewe ni mkristo mpya, hakuna uwekezaji ulio mkuu zaidi unaoweza kufanya katika imani yako zaidi ya kuingiza ndani yako Neno la Mungu mara kwa mara. Anzia hapa ikusaidie Kusoma, Kuelewa na Kutumia kwa ufanisi kila siku. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2