Uwekezaji Wako Ulio Bora!Mfano
“Uhakika wa Mapato!”
Katika ulimwengu wa leo, sentensi hii inafanya mtu astuke na kuleta kushukiwa. Lakini kuna sheria inayofanya kazi karibu katika kila eneo la maisha: sheria ya wakati wa kupanda na kuvuna, au kwa maneno rahisi zaidi, “unavuna ulichopanda.”
Huwezi kuvuna mavuno mpaka kwanza upande mbegu. Huwezi kupata mapato mpaka kwanza ufanye uwekezaji. Huwezi kupata faida ya bidhaa au huduma mpaka kwanza uinunue. Huwezi kuwa na afya bila ya kula chakula bora na kufanya mazoezi. Kwa mifano yote hii, mapato yanayopatikana huendana na ubora wa nguvu iliyotolewa kwanza.
Sheria hiyo hiyo inafanya kazi katika mahusiano yetu na Mungu. Hatuwezi kuvuna maisha ya mwendo wa utoshelevu na baraka na Mungu mpaka pale tunapokuwa tumepanda mbegu zitakazotoa mavuno hayo. Habari njema ni kwamba Mungu ameweka tayari mbegu njema kwa ajili yetu - inaitwa Neno Lake, Biblia. Kupanda kwa ukarimu neno la Mungu katika maisha yetu hutuhakikishia mapato tele katika uwekezaji huo.
Kuhusu Mpango huu
Kupata matunda tele na ya baraka huanzia na kufanya uwekezaji ulio sahihi. Kama wewe ni mkristo mpya, hakuna uwekezaji ulio mkuu zaidi unaoweza kufanya katika imani yako zaidi ya kuingiza ndani yako Neno la Mungu mara kwa mara. Anzia hapa ikusaidie Kusoma, Kuelewa na Kutumia kwa ufanisi kila siku. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2