Injili Ulimwenguni - Sehemu 3Mfano
Hadithi ya nguo mpya na viriba vipya
Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji wakaja na kumwuliza Yesu,
“Imekuwaje kwamba sisi na Mafarisayo tunafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?”
Yesu akawajibu, “Je, wageni wa bwana arusi waweza kuomboleza wakati angali pamoja nao? Wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao, hapo ndipo watakapofunga.
“Hakuna mtu anayeshonea kiraka kipya kwenye nguo kuukuu, kwa maana kile kiraka kitachanika kutoka kwenye hiyo nguo na kuchanika kwa nguo hiyo kutakuwa kubaya zaidi ya hapo mwanzo.
Wala watu hawaweki divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Kama wakifanya hivyo, viriba vitapasuka na divai itamwagika. Navyo viriba vitaharibika, lakini divai mpya huwekwa kwenye viriba vipya na hivyo divai na viriba huwa salama.”
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana.
More
Tungependa kumshukuru GNPI Kenya kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org/