Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Injili Ulimwenguni - Sehemu 3Mfano

Injili Ulimwenguni - Sehemu 3

SIKU 2 YA 7

Yesu aondoa pepo wachafu  

Kisha Yesu akashuka kwenda kapernaumu, mji wa Galilaya na katika siku ya sabato akawa anafundisha. Wakashangazwa sana na mafundisho yake, maana maneno yake yalikuwa na mamlaka.

Ndani ya sinagogi palikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, akapiga kelele kwa nguvu akisema,

"Tuache! tuna nini nawe Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ni mtakatifu wa mungu

Basi Yesu akamkemea yule pepo mchafu, akisema, “Nyamaza na umtoke!”

Yule pepo mchafu akamwangusha chini yule mtu mbele yao wote, akatoka pasipo kumdhuru.

Watu wote wakashangaa wakaambiana, “Mafundisho haya ni ya namna gani? Kwa mamlaka na nguvu, anawaamuru pepo wachafu, nao wanatoka!”

Habari zake zikaanza kuenea kila mahali katika sehemu ile.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Injili Ulimwenguni - Sehemu 3

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana.

More

Tungependa kumshukuru GNPI Kenya kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org/