Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Injili Ulimwenguni - Sehemu 1Mfano

Injili Ulimwenguni - Sehemu 1

SIKU 6 YA 7

  

Siku hizo Yohana Mbatizaji alikuja akihubiri katika Nyika ya Uyahudi, akisema,

“Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni u karibu.”

"Huyu ndiye yule aliyenenwa habari zake na nabii Isaya aliposema,

“Sauti ya mtu aliaye huko nyikani,‘Tayarisheni njia kwa ajili ya Bwana yanyosheni mapito yake.’ ”

Basi Yohana alivaa vazi lililotengenezwa kwa singa za ngamia akiwa na mkanda wa ngozi kiunoni mwake, chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.

Watu walimwendea kutoka Yerusalemu, Uyahudi yote na nchi zote za kandokando ya Mto Yordani.

Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani.

Lakini alipowaona Mafarisayo na Masadukayo wengi wakija ili kubatizwa, aliwaambia, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja?Basi zaeni matunda yastahiliyo toba.

Wala msidhani mnaweza kusemezana, ‘Sisi tunaye Abrahamu, baba yetu.’ Kwa maana nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Abrahamu watoto kutoka katika mawe haya.

Hata sasa shoka limekwisha kuwekwa tayari kwenye mizizi ya mti. Kila mti usiozaa matunda mazuri, hukatwa na kutupwa motoni.

“Mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini nyuma yangu anakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuvichukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Chombo chake cha kupuria kiko mkononi mwake, naye atasafisha sakafu yake ya kupuria, akiikusanya ngano yake ghalani na kuyachoma makapi kwa moto usiozimika.”

Andiko

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Injili Ulimwenguni - Sehemu 1

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana.

More

Tungependa kumshukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: 
http://gnpi-africa.org/