Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waliochaguliwa: Jikumbushe Kuhusu Injili Kila SikuMfano

Chosen: Remind Yourself Of The Gospel Everyday

SIKU 7 YA 7

"Ni Basi, Nayamaliza Yote."


Ujumbe huu ulichipuza katika simu ya rafiki yangu Ryan kutoka kwa namba asiyo ifahamu katika usiku wa Jumanne saa 8:00 usiku. Alikua tu amekaa chili ukumbini mwake baada ya kuwabusu wanawe waende kulala baada ya siku ndefu.

"Samahani, ni nani mwenzangu?" akaurudisha ujembe.

Jina lake lilikua Sara. Sara alifahamu kwamba ametuma ujumbe kwa mtu asiyemfahamu na akamuomba msamaha.

"Ebu gonja dakika moja" Ryan akamrudishia ujumbe. " Naweza saidia."

Waka anza kurudishiana jumbe kwa mda takribani nusu saa. Sara akamueleza Ryan historia yake. Historia ya Sara ilikua inahuzunisha. Kidonda cha mwisho kilikua mpenzi wake wa kiume aliyekuwa anamuacha licha ya tabia yake ya kumnyanyasa. Ryan alijaribu kumjulisha penzi la Yesu Kristo na dhamani yake kwa Mungu licha ya vile Sara alivyokuwa akijihisi. Alimshauri asiyaone maisha yake kupitia maoni ya mpenzi wake mwenye miaka 22.

"Wakati wangu umeisha" Sara akamjibu katika ujumbe, "Nimeshameza chupa nzima ya madawa."

Ryan alimsihi Sara amuelezeke aliko. Ryan alimwambia Sara yeye na mkewe watakuja na kumpeleka hospitali. Sara akamwambia Ryan alipo, na wakamkimbiza hospitali, ambapo madaktari waliweza kumtibu na kunusuru maisha yake.

Kwa miezi iliyofuata, macho ya Sara yalianza kufunguka na kuona alivyo wa dhamana kwa Yesu. Mwishowe Sara alienda chuo kikuu cha kikristo kuufuatilia mpango wa Mungu katika maisha yake. Mungu aliweza kumrehemu, Mungu alichukua maisha yaliyo onekana kukosa maana ulimwenguni - na hata Sara mwenyewe hakuona maana yake - na kuyabadilisha kabisa.Sara alikuwa wa maana sana hata Kristo kufa kwa ajili yake.

Wakati rafiki alikua anapata shahada ya pili katika somo la biashara, mwalimu mkuu katika somo la uchumi aliwawekea wazo kuu: Dhamana ya kitu inabainishwa na malipo mteja anatumai kulipia.

Dhamana iliyolipwa kwa ajili ya dhambi zetu ni damu ya Yesu Kristo, mwana wa Mungu. Je kuna malipo kuliko hayo. Kuna kitu kingine kinachoweza kuiweka dhamana yako juu zaidi ya kitendo hichi?

Sisi sote tunapigana vita kila siku kuiweka dhamana yetu kulingana na malipo Mungu alitoa kwa sababu yetu. Sisi sote tuna sarafu tofauti ya kuipima dhamana yetu. Tunaitumia sarafu ya mafanikio, familia, maumbile, utajiri, utaifa, masomo, uongozi, ushawishi, ama "jaza pengo."

Wanadamu wanajaribu bila mafanikio kuonyesha dhamana ama wanaishi katika msongo wa mawazo kwa sababu wanahisi hawana dhamana.

Hii ndio sababu moja kuu ya kujihubiria neno la Mungu katika nafsi yako. Unaikumbusha nafsi yako dhamana yake katika Kristo kwa kujikumbusha sadaka iliyotolewa ili tuweze kuokolewa.

Andiko

siku 6

Kuhusu Mpango huu

Chosen: Remind Yourself Of The Gospel Everyday

Kutatokea nini kama utaamka kila siku na kijikumbusha juu ya injili? Masomo haya ya siku 7 yanalenga kukukumbusha hilo! Injili si kwamba inatuokoa tuu, bali hutuimarisha pia katika maisha yetu yote. Mwandishi na Mwinjilisti Matt Brown ametayarisha mpango huu wa masomo ambayo yanapatikana katika kitabu chake cha masomo ya siku 30 kilichoandikwa na Matt Brown na Ryan Skoog.

More

Tungependa kuwashukuru Think Eternity kwa kuwezesha mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tembelea tuvuti: https://www.thinke.org