Waliochaguliwa: Jikumbushe Kuhusu Injili Kila SikuMfano
Kanisa moja nchini Urusi lilienda misheni katika kijiji kimoja huko Urusi. Hoja ya misheni yao ilikua kujenga kanisa kutokana na mawe yalilokuwa mwanzoni yametumika kujenga gereza. Ebu tazamia maana ya mandhari hiyo ilivyokuwa kubwa.
Walifanya mankini kuhakikisha wanayaifadhi mawe hayo. Walipokuwa wanatoa jiwe moja kubwa, waliweza kutambua shimo kubwa katika jiwe hilo likiwa na mkebe; na ndani yake kulikua na kibarua kilichosema: "Sisi ni kikundi cha wakristo tunaolazimishwa na wakomunisti tukuchukue mawe ya kanisa letu na tujenge gereza ambapo tutaishi hadi kifo chetu. Maombi yetu ni kwamba siku moja mawe haya kwa mara nyingine yatarudishwa kujenga kanisa."
Wakati Yesu alipofufuka kutoka kwa wafu, Alichagua kujitambulisha kwanza kwa Mary Magdalina. Kwa siku hizo, ushuhuda wa mwanamke haungeweza kuaminika hata kortini. Lakini Yesu alimchagua mwanamke mwenye hadhi ya chini kama shahidi wake wa kwanza, kuonyesha mwanamke wa hadhi ya chini akiwa na ujumbe mwema zaidi ulimwenguni, anaweza kupindua miliki yenye uongozi mkuu katika historia ya wanadamu. Na sasa leo, Ufalme wa Mungu unakua kwa maelfu kila siku, wanaume na wanawake wanampa Yesu maisha yao, na umiliki wa Ufalmwe wa roma hivi leo ni magofu.
Hadithi ya injili ni hadithi ya watu wa kawaida wakishuhudia nguvu kuu za ufufuko. Unapojihisi maskini na bila nguvu, kumbuka Yesu aliyefufuka yuko tayari kuzionesha nguvu zake kukupitia wewe. Maeneo yote katika maisha yako unayohisi umchache ndio haswa Kristo anatazama kufanya muujiza wa kufufua maeneo hayo.
Kristo alifanya miujiza yake mikuu katikati ya watu wa kawaida, katika miji isiyokuwa na umuhimu sana, na katika wakati wa kawaida. Miujiza mingi haikufanya katika hekalu la Yerusalem lakini katika vijiji vilivyokuwa kando kando ya mji huo. Kama upo katika mahali hapana umuhimu, unaweza kuwa upo katika hali njema zaidi ya nguvu za ufufuo wa Mungu kuachiliwa katika maisha yako.
Unapoanza kushiriki injili na moyo wako kila siku, utaanza kuona ufufuko katika siku za kawaida na kila siku, mahali na watu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kutatokea nini kama utaamka kila siku na kijikumbusha juu ya injili? Masomo haya ya siku 7 yanalenga kukukumbusha hilo! Injili si kwamba inatuokoa tuu, bali hutuimarisha pia katika maisha yetu yote. Mwandishi na Mwinjilisti Matt Brown ametayarisha mpango huu wa masomo ambayo yanapatikana katika kitabu chake cha masomo ya siku 30 kilichoandikwa na Matt Brown na Ryan Skoog.
More