Ondoa uogaMfano
Umewahi kupanda ndege na kupitia dhoruba kali angani? Ndege inaweza kuonekana kukosa muelekeo kwa muda, na yawezekana ulipata mashaka kidogo. Kama mkanda wako ulikuwa umefungwa, yawezekana uliukaza zaidi. Yawezekana pia ulijishikiria kwenye kiti kwa nguvu zaidi. Yawezekana ulijisikia kukosa amani kwa sababu kwa muda ulikwa hewani. Yawezekana kama ulikuwa unasoma kitabu ulikuwa unarudia rudia mstari mmoja tu kwa sababu ulivurugwa na dhoruba.
Lakini yawezekana Rubani alitoa tangazo: "Tumeingia kwenye dhoruba, kwa hiyo tutarekebisha urefu ili kupata hali ya hewa iliyotulia." Sasa, tatizo lako halikupotea. Dhoruba bado ilikuwepo. Lakini yawezekana ulivuta pumzi kwa nguvu, ukatulia, ukaendelea kusoma kitabu chako, na yawezekana ukaonekana kutulia zaidi kwa sababu hukujali tena dhoruba na kujali zaidi tangazo la Rubani.
Unapoondoa mawazo yako kwenye kitu unachokiogopa na kuyaelekeza kwa Mungu--yeye anayeyaendesha maisha yetu kwa uhakika--utajisikia hofu yako inatoweka.
Bwana wa neema, ninapokuwa na hofu, nataka kuweka tumaini langu kwako. Naomba unipe mahitaji yangu--mawazo, kweli, na kutiwa moyo--kufanya hivyo? Wewe siyo Mungu wa machafuko, bali Mungu wa amani. Napojisikia sina amani, nimejitenga na uwepo wako. Nitie nguvu ili nikae ndani yako maneno yako yakae ndani yangu, na niweze kupata kikamilifu amani yako. Katika jina la Yesu. Amen.
Umefurahia masomo haya ya kila siku na maombi? Tunapenda kukutia moyo na zawadi ya mahubiri matatu ya Tony Evans kwa kupakua kwenye kiunganishi hiki, ambayo yanaenda ndani zaidi ya tulichojadili leo. Just visit the link here.
Kuhusu Mpango huu
Unaweza kushinda hisia za uoga. Dk. Tony Evans anakuongoza kwenye njia ya uhuru katika mpango huu maalum. Vumbua maisha ya furaha na amani ambayo umekuwa ukiyasubiri unapotumia kanuni zinazoletwa na mpango huu
More