Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ondoa uogaMfano

Get Rid Of Fear

SIKU 2 YA 3

Unafanya nini wakati hofu inaanza kutafuna mawazo yako na haiwezi kukuachia? 

Maandiko yanasema kwamba dawa bora ya hofu na mashaka ni maombi. Kujua nini kinatakiwa na maombi yanaweza kufanya nini juu ya hofu, angalia Wafilipi 4:6–7. Mstari wa 6 unasema, “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.”

Hofu inapokukamata, anza kupambana na hiyo hofu na kweli ya Mungu. Mungu anasema toa mawazo yako kwa sababu chochote kinachotawala mawazo yako, kinakutawala. Mungu hataki uweke mawazo yako kwenye hofu na kutawaliwa nayo. Bali, Mungu anataka umtazame yeye na kuruhusu neno lake na Roho vikutawale. Ndiyo maana maombi ni muhimu sana. Kanuni hapa ni rahisi. Usisumbuke na chochote, bali ombea kila kitu.

Wafilipi 4:6 inatumia neno pana zaidi kuhusu maombi na neno maalum "dua," ambalo lina maanisha kuomba majibu kwa hitaji maalum. Kama una hofu gubu lakini huna uhakika ni juu ya nini, mpelekee Bwana katika maombi--anajua ni nini. Au kama hofu maalum ambayo unaijua akilini mwako, mpelekee nayo pia. Mwombe akusaidie kuiondoa na kuibadilisha na kweli yake, na kisha mshukuru kwa imani kwa kukuondolea.

Bwana wa rehema, mbayuwayu wawili hawauzwi kwa dinari? Na bado unajua kila jambo linalowatokea. Pia unajua idadi ya nywele kichwani mwangu. Nisaidie nipate ujasiri kujua jinsi unavyonifahamu na kunipenda. Nikumbushe leo kwamba sihitaji kuogopa, kwa sababu mwishowe wewe ndiye unayetawala vitu vyote na umeahidi kutokuniacha wala kunipungukia. Asante kwa ahadi zako, ambazo hunipa amani. Katika jina la Yesu. Amen.


siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Get Rid Of Fear

Unaweza kushinda hisia za uoga. Dk. Tony Evans anakuongoza kwenye njia ya uhuru katika mpango huu maalum. Vumbua maisha ya furaha na amani ambayo umekuwa ukiyasubiri unapotumia kanuni zinazoletwa na mpango huu

More

Tungependa kushukuru Harvest House Publishers kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://go.tonyevans.org/addiction