Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano
Ndiyo, unaweza!
Sote hukumbana na majaribu, hii ni sehemu ya maisha ambayo hatuwezi kuepuka. Basi swali si, je utajaribiwa? Bali swali ni, jaribu likija, je utakuwa tayari?
Ningependa uelewe hili; unaweza kushinda majaribu! Acha kusema, “Joyce, sidhani ninaweza” Ondoa neno hilo “siwezi” kwenye maneno yako.
Kwa nguvu na uweza wako, ni kweli, huwezi.Lakini ukiliweka neno la Mungu moyoni mwako, ukitegemea nguvu yake na kuamini ahadi zake, hakuna jaribu litakalo kushinda.
Kwa muda sasa, nimetambua vitu tano vinavyotusaidia kushinda majaribu. Kwanza kabisa, kuwa na hekima. Fikiri kuhusu maamuzi yako na madhara yake kabla ya kutenda jambo hilo. Hekima hukusaidia kuangalia ya mbele.
Pili, inafaa uamini kwamba unaweza kushinda majaribu. Aibu, ghadhabu na kujihukumu hutuzuia, lakini ukikumbana nazo mapema,zinapoteza nguvu zao. Lakini usipozizuia, ni ngumu kuachana nazo. Tatu, ona majaribu haya kama jambo la kawaida. Ikiwa unatarajia vita, basin i bora kuwa tayari. Nne, epukana na yale ambayo unangángána nayo. Usijieke katika hali zinazoweza kukuangusha. Ikiwa kwa mfano unangángána na utumizi wa pesa, usiende kwenye duka la bidhaa ilhali huna pesa za kutumia.
Na ya mwisho, usijione kuwa huwezi anguka. Hatufuzu kutokana na majaribu. Ni rahisi sana kudhani kwamba huwezi kuanguka kamwe, na tunapodhani hivyo, shetani hutafuta hiyo nafasi sana.
Mungu angependa umwamini kukuletea ushindi katika kila eneo la maisha yako. Kwa neema yake…unaweza!
OMBI LA KUANZA SIKU
Mungu nimetambua kuwa majaribu ni sehemu ya masiha yetu. Nisaidie nisije nikagutushwa wakati yanatukia. Asante kwa hekima na neema yako kuweza kushinda majaribu yote na kuishi masiha ya ushindi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi!
More
Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili